Airtel yatangaza punguzo la simu katika wiki ya watoa huduma

Tuesday October 8 2019

 

Kampuni ya Simu za mkononi ya Airtel katika wiki hii ya huduma kwawateja imetangaza kuwa itaendeleza kauli mbiu yao ya ‘Thamani ya mteja ni huduma’ kwa kushusha bei ya simu za Smartphone katika maduka yao yote nchini ndani ya wiki hii.

Mkuu wa kitengo cha huduma kwa Mteja Bi, Adrina Lyamba alisema “Airtel katika wiki hii ya huduma kwa wateja kama kawaida yetu tunaungana na watoa huduma wote katika shamra shamra za wiki yetu ya kutoa huduma inayoadhimishwa duniani kote,

Mwaka huu kauli mbiu ni ‘The Magic of Services’ na kwa Airtel wanasema wameitafsiri kuwa ‘Thamani ya Mteja ni huduma bora’

“Wiki hii tunawatangazia wateja wetu punguzo la simu za mkononi la hadi Sh35,000  ili waendelee kufurahia kuwa ndani ya familia ya Airtel,’ alisema Bi, Lyamba

Aliongeza: Tunalenga kuendelea kuwapa wateja wote huduma bora zaidi na zinazotoa suluhisho la haraka kwa kila hitaji la mteja, alifafanua Lyamba.

Alisema katika kuadhimisha wiki ya huduma, Airtel Tanzania inatoa shukrani  kwa  wateja wote wanaotumia huduma zao.

Advertisement

“Pia tunawakaribisha katika maduka yetu ya huduma kwa wateja zikiwemo Airtel Money Branch zetu zote zaidi ya 1000 nchini  ili kuendelea kujipatia huduma bora ikiwa ni pamoja na kusajili laini kwa mfumo wa alama za vidole au kupata huduma mbali mbali.”

Katika wiki hii ili kujipatia huduma bora kama vile kusajili laini mpya, kujipatia simu na vifaaa vya mawasiliano original kwa bei nafuu na kutakuwa na ofa kabambe maalum.

Advertisement