Jogoo ashinda kesi alipwa Sh 2.4 milioni

Muktasari:

  • Jogoo Maurice ashtakiwa kwa kosa la kuwapigia kelele majirani kwa kuwika, alishinda kesi hiyo baada ya hakimu kulitupilia mbali shitaka hilo na kuagiza alipwe faini ya Sh 2.4 milioni kwa usumbufu.

Ufaransa. Jogoo maarufu kwa sasa  ni Maurice ameshinda shtaka lililokuwa likimkabili la kupigia kelele majirani kila alfajiri na kulipwa fidia.

Corinne Fesseau anaye mmiliki wa jogoo huyo walifikishwa katika Mahakama ya Rochefort nchini Ufaransa Mei, 2019 ili kujibu shtaka lililowakabili.

Mmiliki  huyo amesema jogoo  wake hakuwahi kumkwaza mtu yeyote kabla, huwika muda wowote kama ilivyo kwa jogoo wengine ,  majirani zake walitoa malalamiko kwa mara ya kwanza mwaka 2017 na kumwambia amnyamazishe jogoo huyo.

‘’Tulijaribu kujadiliana lakini hawakutaka kuridhiana kwa njia mazungumzo , tumejaribu kuwaita mara kadhaa wamekuwa wakorofi’’  amesema  Fesseau.

Wakili wa Serikali, Vincent Huberdeau amesema  , ‘’Wateja wangu wanahitaji amani na utulivu katika makazi yao mapya baada ya kustaafu .wanahitaji kulala hadi asubuhi , na wanahitaji jogoo huyo afungiwe wakati wa usiku kama inavyokuwa nyakati za mchana,”amesema

Wakili huyo akaongeza kwamba  “Kazi ya jogoo ni  kuwika asubuhi lakini wateja wangu wapo hapa tangu  mwaka 2003/2004 , jogoo amekuja 2017 ikiwa tayari mji umekua wana nyumba katika eneo la makazi  na sio vijijini  hivyo wanahitaji utulivu’’ .

Baada ya mjadala huo Hakimu, Bruno Dionis du Se’jour alisema kwamba “Jogoo ni alama ya Taifa la Ufaransa , hivyo ni lazima tuwaache wawike  watakapo hitaji’’ , akamalizia kwa kusema kuwa “binadamu hawezi kujibia kwa vitu visivyowezekana’’

Mahakama hiyo imepuuza shtaka hilo na kuwataka walalamikaji kumlipa mmiliki wa jogoo huyo faini ya  kiasi cha euro  1,000 ambazo zinakadiriwa kufikia Sh 2.4 milioni,  kwa usumbufu huku watu 130,000 wakipiga kura mtandaoni kumuunga mkono jogoo huyo.