Kirusi cha ajabu hatarini kusambaa duniani

Sunday January 19 2020

 

Beijing, China. Mamlaka za Afya duniani zimeonyesha wasiwasi kwamba kirusi kilichozuka hivi karibuni katikati ya China kinaweza kusambaa wakati mamilioni ya Wachina watakaposafiri kwa ajili ya sherehe za mwaka mpya wa Kichina.

Ingawa hakuna taharuki kubwa kwenye eneo ambalo kirusi hicho kimeripotiwa lakini baadhi ya watumiaji wa mitandao ya kijamii wamekuwa wakisambaza juu ya taarifa za kirusi hicho kwa njia ya intaneti.

Watu wawili wameripotiwa kufariki dunia hadi kufikia jana asubuhi katika mji wa Wuhan kutokana na mlipuko huo.

Maafisa wa afya wa mji wa Wuhan, China walisema kuwa watu wengine wanne wamethibitishwa kuwa na kirusi hicho.

Taarifa ya wizara ya afya ya China inasema kuwa mgonjwa aliyepatwa na kirusi hicho kinachojulikana kwa jina la Corona kupata homa ya mapafu.

Kwa mujibu wa Shirika la habari la Ufaransa (AFP), mamlaka ya afya nchini China imegundua kirusi hicho kimezuka kutoka soko la vyakula vya baharani lililopo mjini Wuhan.

Advertisement

Advertisement