VIDEO: WHO yapata jina rasmi la ugonjwa wa corona

Wednesday February 12 2020

 

By Emmanuel Mtengwa, Mwananchi [email protected]

Geneva. Shirika la Afya Duniani (WHO) limetangaza jina rasmi la ugonjwa unaosababishwa na maambukizi ya virusi vya corona kuwa ni Covid-19.

Akitoa taarifa kwa waandishi wa habari mjini Geneva, Uswizi Mkurugenzi Mkuu wa WHO, Dk Tedros Ghebreyesus alisema kwa sasa wamepata jina rasmi la ugonjwa huo.

“Sasa ugonjwa huo utafahamika kwa jina la covid-19,” alisema mkurugenzi huyo.

Tangazo hilo linakuja ikiwa tayari ugonjwa huo ambao ulianza mwishoni mwa mwaka 2019 katika mji wa Wuhan, China kusababisha vifo vya zaidi ya watu 1,000.

Tedros alisema co inawakilisha neno corona, vi ikiwa na maana ya virusi, d ikisimama badala ya ugonjwa huku namba 19 ikiwakilisha muda wa utambulisho ambao mlipuko wa ugonjwa huo ulijulikana kwa kwanza mwaka 2019.

Mkurugenzi huy alisema jina hilo limechaguliwa ili kuepusha uhusiano wa eneo, mnyama au kundi la watu.

Advertisement

Advertisement