Wapigakura Hong Kong wafurika kuchagua madiwani

Sunday November 24 2019

 

Hong Kong, China. Wapiga kura mjini Hong Kong leo wamefurika mapema vituoni kupiga kura za kuchagua viongozi wa mabaraza ya halmashauri za wilaya.

Kiasi cha wapiga kura milioni 4 wamejiandikisha kushiriki uchaguzi wa leo,  una unaolenga kuwachagua madiwani 452 wa Baraza la halmashauri katika wilaya 18

Polisi wamesambazwa katika vituo vya kupigia kura ili kuzuia aina yoyote ya ghasia.

Kambi inayopigania demokrasia nchini humo, imesema inatumaini uchaguzi huo utatuma ujumbe kwa serikali ya kisiwa cha Hong Kong kilichopo chini ya China Bara ili isikilize madai yao.

Kisiwa hicho kimekabiliwa na maandamano makubwa na ghasia baina ya polisi na waandamanaji kwa kipindi cha karibu miezi sita sasa.

Jukwaa linaloratibu maandamano hayo limewahimiza raia kupiga kura na kuepusha vitendo vya ghasia, iwapo serikali itaamua kuingilia uchaguzi huo.

Advertisement

 

Misululu ya mamia ya watu ilionekana tangu mapema asubuhi katika vituo cha kupigia kura, hali inayoashiria kuwa wengi watajitokeza kushiriki uchaguzi huo.

 

Serikali ilitangaza kuwa theluthi ya watu milioni 4.13 waliojiandikisha, wamepiga kura katika saa tano za mwanzo, ikiwa ni zaidi ya mara mbili ya wale waliojitokeza katika uchaguzi kama huo mwaka 2015.

 

Uchaguzi wa madiwani ambao hushughulika na kupanga ruti za mabasi na ukusanyaji taka kwa kawaida haukuwa na mvuto, lakini safari hii umevutia wengi kutokana na hali ya maandamano iliyokuwapo.

Uchaguzi huo kwa kawaida uliungwa mkono na wanaotaka China kuikalia Hong Kong, na wapiga kuta wanaotaka mabadiliko wana matarajio ya kuondoa hali hiyo na kupata nguvu mpya ya madai yao.

“Ninatarajia kura hii utaongeza sauti yetu katika halmashauri,” alisema mwanafunzi wa miaka 19, Michel Ng, anayepiga kura kwa mara ya kwanza, alipoongeza na AFP.

Ingawa kura moja inaweza kusaidia kidogo,  bado nina matumaini inaweza kuleta mabadiliko katika jamii na kuunga mkono maandamano mitaani kwa kiasi fulani,” alisema.

Hata hivyo, uchaguzi huo si kwamba hauna maana, Baadhi ya wabunge katika uchaguzi wa mwakani watatokana na madiwani wanaochaguliwa leo na halmashauri hutoa wajumbe 117 katika Bunge la Kitaifa lenye wabunge 1,200 ambalo huchagua mtendaji mkuu.

Maandamano yamesimama mitaani baada ya makundi yanayopigania demokrasia kuwataka wananchi kutulia ili kuepuka kuipa serikali sababu ya kuahirisha uchaguzi huo.

Polisi walitawanywa katika vituo vya kupigia kura na mitaani  lakini si kwa kiwango kikubwa. Hakukuwa na vurugu zozote ziliripotiwa katika saa za awali.

Advertisement