Watanzania wahimizwa kushirikiana na wasadizi wa kisheria kutokomeza ndoa za utotoni

Thursday April 16 2020
tanzani pic

Dar es Salaam. Jamii imehimizwa kushirikiana kuwa karibu na wasaidizi wa kisheria chini ili kuwalinda wasichana na ndoa za utotoni ambazo huchochea umaskini, maradhi na ujinga.

 Meneja Programu wa kitu cha Wasaidizi wa Kisheria mkoani Shinyanga, John Shija alitoa wito huo baada ya kuingilia Kati mpango wa Lyuba Seif na Familia yake wa kumuoza binti yake kati umri mdogo.

 "Kutokana na mkakati huu hatua za haraka zilichukuliwa ili kumnusuru binti huyu asiolewe kwa kulazimishwa akiwa katika umri mdogo na kupoteza kabisa mdoto zake za maisha," alisema.

Ndoa za utotoni zimekuwa ni tatizo kubwa ambalo huwazulumu mabinti wadogo haki zao za msingi katika maisha.

 Wasaidizi wa kisheria katika kila wilaya wamekuwa wakifanya kazi kubwa sana ya kuwasaidia wale wanadhulumiwa haki zao za Kisheria na pia kutoa elimu juu ya masuala mbalimbali ya kisheria katika maeneo hayo.

 Taarifa hizi za mpango wa Seif kumuoza binti yakeziliwafikia watoa huduma za msaada wa kisheria na ilikuwa bahati kwani mpango huu haukuwa umefika hatua ya mbali zaidi.
 
Ili kuzuia mpango huo kuendelea hatua za haraka zilichukuliwa kwa ushirikiano na raia wema katika kijiji hicho.

 Kituo cha PACESHI kilichukua hatua muhimu kumuelimisha Seif juu ya masuala ya Kisheria na haki as watoto na hasa kupata elimu.

 PACESHI ni shirika la wasaidizi wa kisheria chini ya ufadhili wa Legal Services Facility (LSF), shirika linalotoa ruzuku kwa mashiriika yanayotoa huduma za msaada wa kisheria Tanzania Bara na visiwani Zanzibar  chini ya mradi huu Zaidi ya wasaidizi wa kisheria 3700 walioko kila wilaya wameendelea kutoa msaada wa kisheria kwa jamiii. Kwa wastani kwa mwaka wasaidizi wa kisheria ushughulikia takribani zaidi ya kesi 70,000 ambapo asilimia 60 ya kesi hizi wanazitatua wakati asilimia 22 zinakuwa bado zinaendelea, asilimia 16 zimepelekwa kwa vyombo vya juu kwa utatuzi huku asilimia 2 ya kesi zinazowafikia zikishindwa kupatikana usuluhishi.  Kesi zinazotatuliwa kwa wingi na paralegal ni pamoja na kesi za ardhi, ndoa, matunzo kwa watoto, jinai, na ukatili wa kijinsia

 Katika hali hii ambapo ng'ombe watano na kiasi cha laki tatu ilikuwa vimetolewa, kituo cha PACESHI kwa kushirikiana na Wasaidizi wengine wa kisheria walibeba jukumu la kuhakikisha kuwa binti huyu haolewi katika umri mdogo bali anapata ujuzi ambao utaweka msingi katika maisha yake.

 Kituo cha PACESHI kilimuwezesha binti huyu kupata nafasi ya mafunzo ya kushona nguo katika chuo cha VETA mkoani Shinyanga.

 Binti huyu alisema baada ya kuanza mafunzo ya ufundi kuwa yatamuwezesha kufikia ndoto zake za kuwa na maisha bora baadae.

 Kituo cha PACESHI pamoja na wasaidizi wengine  wa Kisheria mkoani Shinyanga walikaa pamoja na wazazi wa binti huyu na kufikia makubaliano ya kumsaidia ili aweze kupata    mafunzo ya ufundi wa kushona nguo.

 Zaidi ya hapo kituo cha PACESHI kiliahidi kumpatia mtaji  wa kuanzia pale  atakapokuwa amehitimisha  mafunzo yake ili aweze kuanzisha biashara ya kushona nguo ikiwa pamoja na kununua mashine ya kushona nguo.

 Kwa upande wake Theresia Masinga, manage ni mwalimu wa chuo cha VETA Shinyanga alisema tangu siku ya kwanza binti huyu alipoanza mafunzo ameonyesha bidii kubwa sana na kuwa jitihada hizi ni kiashiria  cha malengo  aliyojiwekea katika maisha.

 Mzee Seif anawakilisha sehemu ndogo sana ya mabinti Wengi ambao wamekuwa wakidhulumiwa haki zao za msingi za kupata elimu.

Advertisement