Breaking News

Miili ya watu watano wa familia moja waliopoteza maisha kuwasili leo Sengerema

Sunday October 18 2020

 

Buchosa.Miili wa watu wa familia moja waliopoteza maisha Jijini Dar es salaam inatajia kuwasili leo Wilayani Sengerema  Mkoa wa Mwanza kwa ajili ya maziko ,na maziko hayo yanatajia kufanyika kesho Kijiji cha Sukuma kata ya Bukokwa Halmashauri ya Buchosa Wilayani Sengerema.

Ofisa Mtendaji Kijiji cha Sukuma Simoni Faida amethibitisha kuwa miili hiyo itawasili leo na tayari taratibu za maziko zinaendelea kufanyika Kijiji hapo.

Watu hao walipoteza maisha kwa kukosa hewa ya oksijeni  Oktoba 13, baada ya nyumba waliyokuwa wamelala usiku kupata hitilafu ya umeme na kuungua.

Waliopoteza maisha  katika moto huo ni Jackline Frank ambaye ni mkewe, Esther mwenye miaka 15 (mdogo wake na mwanafunzi wa kidato cha nne sekondari ya Pugu Station) pamoja na watoto wake watatu; Edwin (mwanafunzi wa shule ya msingi Pugu Station, Edison (Green Hill) na Ivon mwenye umri wa miaka minne.

Mmoja wa kazi wa Kijiji cha Sukuma Kata ya Bukokwa Wilayani humo Tungalaza Kazimili amesema nimsiba mzito ambapo hauwezi kuvumilika katika Kijiji hicho.

Advertisement