Beki wa Real Madrid atua Tanzania, atembelea Hifadhi ya Serengeti

Wednesday June 5 2019

Staa ,Real ,Madrid , Serengeti , Mpenzi ,Beki , Real, Madrid, atua, Tanzania

By Evagrey Vitalis, Mwananchi [email protected]

Dar es Salaam. Si ajabu kuona wageni wakifika Tanzania kutembelea hifadhi mbalimbali za Taifa ikiwa ni moja ya mafaniko ya Serikali kutangaza vivutio hivyo vya utalii.

Miongoni mwa watalii waliotua Tanzania kushuhudia vivutio hivyo ni beki wa klabu ya Real Madrid ya nchini Hispania, Theo Hernandez (21) anayecheza kwa mkopo

klabu ya Real Sociedad inayoshiriki Ligi Kuu ya Hispania kama ilivyo Real Madrid.

Mchezaji huyo ameweka picha katika mtandao wake wa kijamii wa Instagram akionekana kuwa katika Hifadhi ya Taifa ya Serengeti pamoja na mpenzi wake.

Wachezaji mbalimbali wakiwemo waliostaafu soka kwa nyakati tofauti wametembelea Hifadhi za Taifa nchini akiwemo staa wa zamani wa Manchester United na Real Madrid, David Beckham aliyeongozana na wanawe na mkewe, Victoria.

Real Sociedad ilimaliza katika nafasi ya tisa katika ligi hiyo ikiwa na pointi 50. Klabu ya Barcelona ndio mabingwa wa msimu wa 2018/2019.

Advertisement

Advertisement