CCM yabeba Majimbo yote Magharibi B

Muktasari:

CCM yaibuka kidedea kwenye nafasi ya uwakilishi katika majimbo yote matano ya Wilaya ya Magharibi B,  Unguja.

Unguja. Msimamizi wa uchaguzi Wilaya ya Mjini Magharibi B Unguja, Fatma Gharib Haji, ametangaza matokeo ya nafasi ya uwakilishi katika majimbo yote matano ya wilaya hiyo ambayo wagombea kutoka CCM wameshinda.

Fatma ametangaza matokeo hayo leo Alhamis Oktoba 29, 2020 akisema katika jimbo la Pangawe, aliyeshinda ni Ali Suleiman  Ameir kwa kura 5, 471 dhidi ya Suleiman Simai 3,218 wa  ACT-Wazalendo.

Wakati katika jimbo la Mwanakwerekwe Ameir Abdallah wa CCM amepata kura 9,942 dhidi ya AbdilahJihad Hassan 2,962. Katika jimbo la Kiembesamaki - Suleiman Haroub wa CCM amepata kura  8,151 dhidi ya Ali Suleiman Hassan wa ACT Wazalendo aliyepata  kura 1,807

Kwa mujibu wa Fatma, jimbo la Dimani  mshindi ni Mwanaasha Khamis wa CCM aliyepata  kura 11359 dhidi ya Zahra Ally wa ACT Wazalendo aliyepata kura 2,704.

Huku Yusuf Hassan wa CCM akiibuka mshindi katika jimbo la Fuoni kwa kupata kura  6,895 na Juma Rajab wa ACT alipata kura  1, 551.