Dk Shoo achaguliwa kuwa mkuu wa kanisa KKKT

Saturday August 24 2019

 

By Mussa Juma, Mwananchi [email protected]

Arusha. Dk Frederick Shoo amechaguliwa tena kuwa mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) baada ya kupata kura 144 dhidi ya 74 za mpinzani wake.

Kwa ushindi huo, Dk Shoo anaendelea kuliongoza kanisa hilo kwa miaka mingine minne na kufuata nyayo za wakuu wa kanisa hilo waliomtangulia walioliongoza kwa vipindi viwili vya miaka minne.

Ametangazwa kuwa mshindi usiku wa kuamkia leo Jumamosi Agosti 24, 2019 baada ya kumalizika kwa uchaguzi uliofanyika mjini Arusha na kutawaliwa na kila aina ya upinzani.

Alipata kura 144 kati ya 218 huku mpinzani wake Askofu Abednego Keshamshahara wa Dayosisi ya Kaskazini Magharibi akipata kura 74.


Advertisement