Jela miaka 20 kwa kumuingiza uume mdomoni, njia ya haja kubwa

Muktasari:

Liziki Kessy mkazi wa Kimara jijini Dar es Salaam amehukumiwa kwenda jela miaka 20 baada ya kukutwa na hatia ya kumuingiza uume mdomoni aunyonye na njia ya haja mtoto wa kiume mwenye umri wa miaka saba.

Dar es Salaam. Mahakama ya Wilaya ya Kinondoni Dar es Salaam imemuhukumu kifungo cha miaka 20 jela mkazi wa Kimara Stop Over, Liziki Kessy baada ya kukutwa na hatia ya kumwingiza uume wake kwenye haja kubwa na mdomoni mtoto wa kiume mwenye umri wa miaka saba ili aunyonye.

Hukumu hiyo imesomwa leo Jumatatu Januari 20, 2020 na Hakimu Mkazi, Hudi Hudi amesema mahakama hiyo imemtia hatiani mshtakiwa huyo baada ya kupitia mashahidi watano wa upande wa mashtaka  huku upande wa utetezi ukiwa na  mashahidi watatu akiwamo mshtakiwa mwenyewe.

Hudi amesema amezingatia shtaka hilo adhabu ya chini  ni miaka 30 hivyo mahakama hiyo  imemuhukumu mshtakiwa huyo  kwenda jela miaka 20 .

Hudi amesema baada ya kupitia upande wa ushahidi wa mashtaka na ushahidi upande wa utetezi mahakama hiyo imebaini mshtakiwa huyo alimfanyia tendo la aibu kwa mtoto huyo.

Amesema kutokana na mtoto (muathirika) huyo kuieleza mahakama jinsi mshtakiwa alivyomwita na kumpeleka kwenye jumba  bovu huku akimvua kaptura na kuanza kumuingizia uume wake kwenye haja kubwa na alipopiga kelele ndipo mshtakiwa huyo aliuingiza uume kwenye mdomo wa mtoto huyo.

"Ushahidi wa muathirika umeungana na ushahidi aliyoutoa mama yake mzazi pamoja na daktari wa hospitali ya Rufaa ya Mwananyamala ambaye alibaini mtoto huyo alikuwa na michubuko kwa jinsi ilivyo kama kuna kitu kisicho na ncha kimeingizwa sehemu  ya haja kubwa," amesema Hudi.

Kutokana na hilo mahakama  imeona mambo hayo yamethibitika hivyo mshtakiwa anatiwa hatiani kwa shtaka la kumwingiza uume wake kwenye haja kubwa na  mdomoni  mtoto huyo.

Wakili wa Serikali, Dasy Makakala alidai mshtakiwa huyo apewe adhabu kali kwa kuwa watoto wanadhalilishwa na kubakwa ili iwe fundisho kwa watu wenye tabia hiyo.

Naye mshtakiwa huyo alidai yeye ni muathirika ana ugonjwa wa kisukari na kifua kikuu (TB) na anatumia dawa hivyo asipewe adhabu kali na hana wazazi yeye ni yatima.

Kesi ya msingi mshtakiwa anadaiwa kutenda kosa kosa la shambulio la aibu, Julai 24 mwaka 2018 maeneo ya Kimara Stop Over mshtakiwa alimwingizia uume wako mdomoni na haja kubwa mtoto wa kiume wa miaka saba