Kiongozi wa Korea Kaskazini aibua ubashiri na picha ya farasi mweupe

Muktasari:

Wachunguzi wa mambo wanasema huenda picha hiyo inaashiria kuwa kutakuwa na uamuzi mkubwa kwa taifa hilo lililo na silaha za nyuklia.


Seoul, Korea Kaskazini (AFP). Picha mpya ambayo haijaonyesha ilichukuliwa lini na inayomuonyesha Kim Jong Un wa Korea Kaskazini akiwa amepanda farasi mweupe katika maeneo ya barafu ya Mlima Paektu, imeibua ubashiri kuwa huenda kiongozi huyo kijana akatangaza jambo kubwa.

Picha hiyo iliyotolewa na shirika la habari la KCNA inamaanisha kuwa kiongozi huyo anaendesha jambo ambalo lina umuhimu mkubwa kwa taifa hilo.

Viongozi walioongozana naye walibakia wakishawishika kuwa "kutakuwa na operesheni kubwa nyingine itakayoikumba dunia na ambayo itaendeleza mapinduzi ya Korea Kaskazini," shirika hilo la habari lilisema.

Wachambuzi wanasema picha hiyo inaweza kuwa inatuma ujumbe kuwa kuna mwelekeo mpya wa sera kwa taifa hilo lenye silaha za nyuklia.

"Zamani, Kim alipanda Mlima Paektu kabla ya kufanya uamuzi mkubwa wa kisiasa," alisema Shin Beom-chul, mchambuzi kutoka Taasisi ya Masomo ya Sera ya Asan.

Kim alipanda mlima Desemba 2017 kabla ya kuanza harakati zilizomalizika kwa kuwa na mkutano wa kwanza wa viongozi wa nchi baina yake na Rais Donald Trump wa Marekani.

Lakini mazungumzo hayo yamekumbana na kikwazo tangu mkutano wa pili baina ya Kim na Trump ilipovunjika mwezi Februari na Korea Kaskazini imekuwa ikiendeleza taharuki kutokana na kufanya majaribio mfululizo ya makombora yake ya msafa marefu.

taswira ya kiongozi huyo akiwa juu ya farasi mweupe katika maeneo ya mlima yenye barafu, hasa Mlima Paektu - imekuwa ni ujumbe uliotawala picha za zamani na mabango ya Kim Il Sng ambaye ni baba yake Kim Jong Un.

Kwa mujibu wa B.R. Myers, profesa katika Chuo Kikuu cha Dongseo cha Korea Kusini ambaye amejikita katika propaganda za Korea Kaskazini, picha hizo zinawakilisha taswira ya kiongozi anayetaka kulinda utamaduni na itikadi ya taifa lisilo na rushwa.

Kim pian alitembelea maeneo ya miradi mikubw aya ujenzi karibu na kaunti ya Samjiyon, kwa mujibu wa KCNA na kulaumu kuwa ugumu wa maisha katika nchi yake umesababishwa na vikwazo ilivyowekewa vinavyotokana na ushawishi wa Marekani.