Magufuli amteua Diwani kuwa bosi Usalama wa Taifa

Thursday September 12 2019

Rais wa Tanzania, John Magufuli,Dk Modestus Kipilimba,Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Usalama wa Taifa kuchukua nafasi ya Dk Modestus Kipilimba

 

By Mwandishi Wetu, Mwananchi [email protected]

Dar es Salaam. Rais wa Tanzania, John Magufuli amemteua na kumuapisha Diwani Athuman kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Usalama wa Taifa kuchukua nafasi ya Dk Modestus Kipilimba.

Taarifa iliyotolewa leo Alhamisi Septemba 12, 2019 na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu, Gerson Msigwa inaeleza kuwa uteuzi wake umeanza leo.

Kabla ya uteuzi huo,  Diwani aliyeapishwa Ikulu, Dar es Salaam leo alikuwa mkurugenzi mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru).

Akizungumza baada ya kumuapisha, Rais Magufuli amemtaka kuchapa  kazi kwa juhudi na maarifa na kuweka mbele maslahi ya Taifa.

Taarifa hiyo inaeleza kuwa Kapilimba atapangiwa kazi nyingine.

 

Advertisement


Advertisement