Mapambano dhidi ya malaria yaelekezwe katika ngazi ya jamii

Maadhimisho ya Siku ya Mbu Duniani yaliyofanyika hivi karibuni, yalilenga kukuza ufahamu kuhusu namna za kuzuia malaria, lakini swali ni kwamba nini kifanyike ili kumaliza kabisa ugonjwa huo?

Katika mahojiano haya, ofisa mtendaji mkuu wa Harakati ya Kitaifa ya Kupambana na Malaria Tanzania (TANAM), Beatrice Minja ambaye amekuwa kwenye mapambano dhidi ya malaria kwa zaidi ya miongo miwili, anaelezea umuhimu wa kushirikisha watu au jamii kwa ujumla katika harakati zote za kutokomeza malaria.   

Mwandishi: Kwa zaidi ya miaka 20 iliyopita umekuwa kwenye kampeni dhidi ya malaria. Je, nini tathmini yako kuhusu mapambano dhidi ya ugonjwa huo unaoendelea kuenea hadi leo?

Minja:  Mwaka 2002, malaria ilikuwa ni tatizo kubwa lakini swala hili halikuzungumziwa sana wakati ule. Wakati huo kulikuwa na uwekezaji mdogo sana, lakini baada ya miaka mingi ya kushawishi Serikali pamoja na watendaji wengine leo tunaona uwekezaji zaidi ukiongezeka ili kusaidia kupambana na ugonjwa huo.  Mapambano haya yanaweza kuzaa matunda zaidi tukiwekeza katika  kushirikisha jamii kukuza mapigano hii.

 Mwandishi: Kwa nini jamii ishiriki? Je, hazijashiriki kikamilifu katika mapambano dhidi ya malaria nchini?

Minja:  Sitasema jamii haijashiriki kikamilifu. Ni kwa sehemu tu. Kumekuwa na ushiriki fulani. Hatua nyingi zilizochukuliwa sasa dhidi ya malaria kimsingi si za kijamii. Programu kama za ugonjwa wa malaria hazitokani na watu wenyewe, zinatika juu; ama serikalini au wadau wa maendeleo.Ikiwa jamii hazijui mipango ya ugonjwa wa malaria hiyo inamaanisha kuwa kujitolea kwao katika kupambana na ugonjwa huo kupo chini sana.

 

Mwandishi:  Nini kinaweza kubadilika ikiwa jamii zitajishughulisha kikamilifu katika kukabiliana na malaria?

Minja: Kama tutashirikisha jamii, watatumia ubunifu wao na watakuwa na maarifa mapya ya namna ya kukabiliana na malaria. Hii pia imeonyeshwa katika udhibiti wa wadudu, watu huwa wanangojea Serikali kutekeleza zile hatua katika maeneo yao. 

Mwandishi: Nini kinachohitaji kubadilika ikiwa Tanzania inapaswa kuweka jamii katikati ya mapambano dhidi ya malaria?

Minja: Wananchi wanahitaji kuelewa kuwa ni jukumu lao kushughulikia changamoto zao za kiafya na si kungojea mtu mwingine. Kwa hivyo, tunahitaji kuboresha mifumo ya kijamii.

Mwandishi: Umeshiriki katika mipango ya kudhibiti ugonjwa wa malaria kupitia TANAM. Je! Umefanya nini ili kupunguza kiwango cha kuenea kwa malaria nchini?

Minja:  Mtazamo wetu tangu mwanzo umekuwa ni kutokomeza malaria. Tulielewa kuwa kama shirika moja tusingefanikiwa. Kwa hivyo, tulihamasisha mashirika yasiyo ya kiserikali, mashirika yaliyosimamiwa na jamii (CBOs), mashirika ya dini na vikundi vingine kupata sauti moja tunayohitaji kushinikiza ajenda ya ugonjwa wa malaria.

Kupitia sauti hiyo, tumeweza kuishauri Serikali ichukue njia gani ya kupambana na malaria.

Mwandishi: Nini ambacho wewe (kama TANAM) bado haujakifanya na unahitaji kufanya katika mapambano ya ugonjwa wa malaria?

Minja:  Jambo linalofuata ambalo tunataka kufanya ni kusisitiza kwamba Tanzania ianze kuzalisha dawa ya malaria ambayo ni ya kipaumbele. Hatujapata nafasi hii na ninaamini kama nchi tunaweza kuifanya. Kwa kuwa na bidhaa zetu wenyewe, tunaunda ajira kwa watu wetu tunatumia maliasili zetu wenyewe.

Mwandishi: Je! Unafikiri ni nini bado kinakwamisha juhudi za kutumia rasilimali zetu wenyewe kutengeneza dawa za kupunguza ugonjwa wa malaria? 

Minja: Changamoto hapa ni ukosefu wa uwekezaji. Ikiwa Serikali itaangalia suala hilo, pengine watafute washirika ili kufanikisha kufanya hivyo, inaweza kuwa bora zaidi. Kuna ushindani mkubwa katika eneo hilo, najua, lakini yote yanaweza kufanywa. Hii yote itategemea ikiwa Serikali itafanya iwe kipaumbele.

Mwandishi: Tukichukulia mfano kiwanda cha Kibaha cha kuua vimelea vya mbu ambacho kilizinduliwa takriban miaka mitatu iliyopita hapa nchini. Je! Unafikiri sisi kama nchi tumeutumia kikamilifu?

Minja: Hapana. Nchi haijatumia kikamilifu kwa sababu hatuoni bidhaa zake kwenye soko. Sisi kama TANAM, tulikwenda kiwandani kilipozinduliwa na tulitaka kujua jinsi mkakati wake wa uuzaji utakavyokuwa na pia kujua sehemu yake ya soko inayoweza kupatikana kwa Tanzania. 

Lakini, tangu wakati huo, hatujaona bidhaa kwenye soko hata kama tuna soko letu la ndani. Je! Kwa nini hatutumii bidhaa?  Tunaona kuwa hakukuwa na mkakati wa uuzaji na kama hakuna hilo, inamaanisha kwamba msambazaji hajulikani. Tulienda mbele na kupima kama jamii ina uwezo wa kuitumia. Tuligundua kuwa jamii iko tayari na inaweza kuitumia.

Mwandishi: Je! Unafikiri Serikali kwa sasa inachukua njia sahihi katika kudhibiti malaria?

Minja: Kinadharia, serikali ina mkakati mzuri wa kupambana na malaria ambao unaongoza programu hizo, lakini ndani ya mkakati huo, kuna sehemu chache ambazo hazijafanyiwa kazi. Kwa mfano, hivi sasa kuna kampeni Zaidi kuhusu utumiaji vyandarua. Imesaidia, lakini vyandarua haviwezi kutokomeza malaria.Kumekuwa na matumizi ya tiba na tunaona mafanikio katika hili, lakini tunahitaji mchanganyiko wa mikakati sasa. 

 Tunapotazamia kumaliza ugonjwa wa malaria ifikapo 2030, Serikali iatazame kwa upya jinsi tunavyoshirikisha watu, washirika na sekta zingine.

Mwandishi: Umefanya kazi ya kupambana na malaika huko Zanzibar. Ukiangalia maendeleo ambayo yametekelezwa katika kisiwa hicho, unafikiria Zanzibar huweka nini mbele ili kuthibiti ugonjwa wa malaria

Jibu: Zanzibar ni Kisiwa. Ni eneo dogo ukilinganisha na bara ambako suala la ugonjwa wa Malaria linaweza kuwa gumu sana. Bara pia limefanya mengi sana. Sehemu kubwa ya nchi imepunguza ugonjwa wa malaria lakini kuna maeneo ambayo yanahitaji kazi kubwa, kama Ukanda wa Pwani. Tunaona kwa umakini kuwa ukanda wa Pwani ni hatari sana. Je! Kwa nini hatuwezi kuweka kazi kubwa zaidi huko? Navyoona ni kwamba maambukizi huja kutoka kwa maeneo haya ya Pwani na maziwa.

Kuna kampeni zinazoendelea katika maeneo hayo kwenye matumizi ya vyandarua na hatua zingine kama vile dawa ya kupulizia mabaki ya ndani. 

Hizi zinasaidia. Tunatumaini zaidi itafanyiwa pia Lindi, Ruvuma, Mtwara na Pwani; katika ukanda wa Pwani kwa ujumla juhudi nyingi zinahitajika sana.

Mwandishi: Ikiwa leo mtunga sera akakukaribia na kukuomba upendekeza njia moja bora ya kukabiliana na hali ya ugonjwa wa malaria nchini, ungeshauri nini?

Minja:   Ningemwambia azingatie kwa umakini mikakati ya kudhibiti wadudu ambayo inashughulika na mbu. Kwa kweli ningewaomba walifanyie kazi kwa umakini zaidi. Na kwamba tuliangalie hili swala kitaifa na kwa ujumla. Kinachoweza kufanywa bora ni kuweka sera ambayo itaongoza jinsi hii inaweza kufanywa katika makazi ya mijini na mahali ambako kuna msongamano mkubwa wa wadudu. Suala hapa ni kuifanya shuguli hii iwe ya kipaumbele Viongozi wa mitaa wanaweza kusukuma ajenda kuwafikishia jamii. Serikali ianzishe idara katika wizara ya afya ambayo itashughulika na wadudu wanaoeneza magonjwa kwa binadamu