Mbunge CCM afariki dunia

Wednesday January 15 2020

 

By Muyonga Jumanne, Mwananchi [email protected]

Dar es Salaam. Mbunge wa Newala Vijijini (CCM), Rashid Akbar amefariki dunia leo Jumatano Januari 15, 2020 mkoani Lindi.

Taarifa iliyotolewa leo  na ofisi ya Bunge la Tanzania inamnukuu  Spika Job Ndugai akieleza kuhusu kifo cha mbunge huyo, kutoa pole kwa wafiwa.

Inaeleza kuwa mipango ya mazishi inaendelea kuratibiwa na ofisi ya Bunge kwa kushirikiana na familia ya mbunge huyo.

“Natoa pole kwa wafiwa wote wakiwemo familia ya marehemu, wabunge, ndugu, jamaa na marafiki. Mungu awape uvumilivu katika kipindi hiki kigumu,” amesema Ndugai.

Awali taarifa ya katibu wa siasa na uenezi wa CCM mkoani Mtwara, Seleman Sankwa ilieleza kifo cha mbunge huyo.

“CCM inathamini na kutambua mchango mkubwa wa marehemu enzi ya uhai wake akiwa mbunge katika kuwatumikia wananchi wa Newala vijijini,” amesema  Sankwa.

Advertisement

Advertisement