Mkazi Tanga akamatwa na gramu 500 za dawa za kulevya

Monday February 17 2020

Mkazi wa barabara ya 19 Jijini Tanga Hamad

Mkazi wa barabara ya 19 Jijini Tanga Hamad Mbaraka anayetuhimiwa kukutwa na gramu 500 za dawa za kulevya aina ya Heroine kufuatia oparesheni iliyoongozwa na Kamishna General wa tume ya kudhibiti na kupambana na dawa za kulevya James Kagi saa 6 usiku wa kuamkia leo jumatatu 

By Pamela Chilongola, Mwananchi [email protected]

Tanga. Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya Tanzania (DCEA) imemkamata Hamad Mbaraka kwa tuhuma  za kukutwa na gramu 500 za dawa za kulevya aina ya Heroin.

Mtuhumiwa huyo mkazi wa barabara ya 19 Wilaya ya Tanga mjini  amekamatwa usiku wa kuamkia leo Jumatatu Februari 17, 2020.

Akizungumza leo kaimu Kamishna Jenerali wa DCEA, James Kaji amesema mtuhumiwa huyo alikamatwa saa 6 usiku, “alikuwa amezificha katika mfuko  mmoja wa plastiki ndani yake kulikuwa na pakiti tatu tofauti zilizokuwa na dawa hizo.”

“Tangu saa 2 usiku jana tulikuwa tunamtafuta mtuhumiwa, tulikuwa tunafanya mawasiliano ila ilipofika saa 6 usiku tulimkamata, kwa sasa yupo mahabusu anaendelea kuhojiwa.”

Amesema wamepeleka kithibitisho hicho kwa mkemia mkuu wa Serikali kwa ajili ya kupimwa.

Amebainisha kuwa katika mahojiano mtuhumiwa huyo amekiri kuwa anapopatiwa dawa hizo huzificha kwenye mashamba eneo la Pangani.

Advertisement

Advertisement