Pato la kila Mtanzania laongezeka kwa Sh 100,000

Muktasari:

Waziri wa Fedha na Mipango Dk Philip Mpango amewasilisha bungeni jijini Dodoma taarifa ya hali ya uchumi wa Taifa mwaka 2018 na Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa mwaka 2019/2020, kubainisha kuwa pato la kila Mtanzania limeongezeka kutoka Sh2.3 milioni mwaka 2017 hadi Sh2.4 milioni mwishoni mwa 2018.


Dodoma. Serikali ya Tanzania imesema pato la wastani la kila Mtanzania lilifikia Sh2.4 milioni mwishoni mwa mwaka jana kutoka Sh2.3 milioni mwaka 2017.

Hayo yameelezwa leo Alhamisi Juni 13, 2019 na Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Philip Mpango  wakati akiwasilisha bungeni jijini Dodoma taarifa ya hali ya uchumi wa Taifa katika mwaka 2018 na Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa mwaka 2019/2020.

Dk Mpango amesema ongezeko hilo ni sawa na wastani wa asilimia 5.6. Kutokana na takwimu hizo, ongezeko hilo ni sawa na Sh100,000 kwa kila Mtanzania

Dk Mpango amesema kiasi cha pato la wastani kwa kila mtu mwaka 2018 ni sawa na Dola 1,090 za Marekani ikilinganishwa na Dola 1,044 za Marekani  mwaka 2017, sawa na ongezeko la asilimia 4.4.