Polisi Tanzania yawakamata waliokuwa vigogo bodi ya kahawa

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro, Salum Hamduni 

Muktasari:

  • Watu wanne ambao waliokuwa vigogo wa Bodi ya Kahawa Tanzania (TCB) wanashikiliwa na Jeshi la Polisi mkoani Kilimanjaro nchini Tanzania kwa tuhuma za wizi wa fedha zaidi ya Sh2 bilioni.

Moshi. Polisi Mkoa wa Kilimanjaro nchini Tanzania linawashikilia watu wanne waliokuwa viongozi wa Bodi ya Kahawa Tanzania (TCB) kwa tuhuma za wizi wa fedha kiasi zaidi ya Sh2 bilioni.

Akizungumzia kukamatwa kwa watuhumiwa hao leo Jumatatu Novemba 25, 2019, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro, Salum Hamduni amesema vigogo hao walikamatwa juzi Jumamosi Novemba 23, 2019.

"Ni kweli Jeshi la Polisi Kilimanjaro linawashikilia watuhumiwa wanne kwa tuhuma za wizi wa fedha kiasi cha Usd 908,065.65 mali ya Tanzania  Coffee Board (TCB)," amesema Hamduni

Aidha amesema fedha hizo zinadaiwa kuibiwa kwa nyakati tofauti katika msimu wa mauzo ya Kahawa mwaka 2016/2017 na 2017/18.

Hamduni amesema upelelezi wa kukamatwa kwa vigogo hao unaendelea na kwamba  utakapokamilika jalada litawasilishwa Ofisi ya Taifa ya Mashtaka na taratibu za kuandaa hati ya mashtaka ili watuhumiwa wafikishwe mahakamani.

Kamanda Hamduni ametaja majina yao kuwa ni Astery Bitegeko, aliyekuwa mkurugenzi wa Fedha,  Goodluck Moshi, alikuwa mhasibu mwandamizi, Isaya Mrema, aliyekuwa mkaguzi wa ndani pamona na Emaculate Bitegeko