Polisi yamshikilia mume anayedaiwa kumuua mkewe, kumtupa migombani

Muktasari:

  • Mkazi wa Arusha, Amir Hassanm anashikiliwa na Polisi kwa tuhuma za kumuua mkewe, Lidya Kiwale kisha mwili wake kuutupa katika migomba jirani na makazi yake.

Arusha. Polisi Mkoa Arusha nchini Tanzania linamshikilia Amir Hassan kwa tuhuma za  kumuua mke wake, Lidya Kiwale usiku wa kuamkia leo Jumapili Septemba 15, 2019.

Tukio hili ni mfululizo wa matukio ya wanawake kuuawa kikatili katika mji wa Mto wa mbu ambayo yamedumu kwa zaidi ya miaka mitatu ambapo wanawake 11 wameuawa.

Akizungumza na Mwananchi leo Jumapili Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, Jonathan Shana amesema tukio hilo limetokea kijiji cha Majengo  na baada ya mauaji hayo Hassan anatuhumiwa kutupa mwili kwenye migomba jirani na makazi yake.

"Tumepata taarifa za tukio hili ambalo limetokea usiku wa kuamkia leo (Jumapili) na mtuhumiwa tayari ameshikiliwa na polisi kwa mahojiano, “amesema.

Amesema uchunguzi ukikamilika mtuhumiwa huyo atafikishwa mahakamani.

Endelea kufuatilia Mwananchi kwa habari zaidi