Sauti za Busara yaungana na CRDB kutangaza utalii Zanzibar

Zanzibar.  Benki ya CRDB wikiendi hii iliibuka kuwa mdau muhimu katika kufanikisha tamasha kubwa la kila mwaka la kimataifa la Zanzibar lijulikanalo kwa jina la “Sauti za Busara”. Akizungumza katika ufunguzi wa tamasha hilo mjini Zanzibar juzi, Mkurugenzi wa Tamasha hilo Bwana Yusuph Mohamed alisema  kuwa udhamini na uwepo wa Benki ya CRDB katika tamasha la mwaka huu umeleta hamasa kubwa katika kulitangaza zaidi tamasha hilo na pia kuhakikisha kuwa huduma za benki zinapatikana kwa wahudhuriaji wa tamasha hilo. “Tuna furaha kuwa Benki kubwa kama CRDB imejitiokeza na kuunga mkono tamasha hili ambalo linalenga kuibua vipaji, kutoa ajira na kuboresha utalii wa ndani. Kikubwa zaidi tunafurahishwa na kitendo cha Benki  ya CRDB kuweka banda maalum la kutolea huduma za uwakala na ubadilishaji fedha za kigeni kwa washiriki wa tamasha hili” alisema  Mohmoud.

Kwa upande wake Mkuu wa Kitengo cha biashara ya kadi cha Benki ya CRDB Bwana Farid Seif, alisema kuwa benki hiyo iliamua kudhamini  tamasha hilo ili kuunga mkono juhudi za kutangaza vivutio vya utalii nchini na kuibua vipaji vya sanaa ambavyo ni sehemu kubwa ya ajira kwa vijana.
Bwana Farid alisema pia ili kunogesha ushirki na ufahamu   juu ya  tamasha hilo, Benki ya  CRDB kupitia kampeni ya malipo kwa kadi ijulikanayo kwa kama “Scan, Chanja, Lipa Sepa,’ imedhamini wateja wanne kushiriki tamasha hilo kwa kuwalipia gharama zote za usafiri na malazi kwa sika tatu za tamasha hilo. “Tunaendelea kuwahamasisha wateja wetu kufanya manununzi na malipo kwa kutimia kadi zao katika mashine zetu za malipo yaani POS, zilizopokatika  kila kona ya nchi  ndani ya maduka, vituo vya mafuta, migahawa na sehemu mbalimbali za huduma na hivyo kuachana na utaratibu wa kutembea na pesa nyingi taslimu," alisema Farid.