TMA yatabiri mvua kubwa mikoa minne Tanzania

Muktasari:

Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania ( TMA)  imetoa utabiri wa hali ya hewa kwa siku tano na kubainisha mikoa itakayonyesha mvua kwa kipindi hicho ambayo ni Lindi, Mtwara, Ruvuma na kusini mwa Morogoro.

Dar es Salaam. Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania ( TMA)  imetoa tahadhali ya mvua kubwa itakayonyesha katika mikoa ya Lindi, Mtwara, Ruvuma na kusini mwa Morogoro leo Jumatano Januari 22, 2020.

Pia, TMA imetoa tahadhali ya upepo mkali na mawimbi makubwa katika mikoa ya Lindi, Mtwara, Pwani, Dar es Salaam, Tanga pamoja na visiwa vya Unguja na Pemba.

Taarifa ya TMA iliyotolewa jana Jumanne Januari 21,2020 inasema mvua hizo zitaanza mvua hizo zinaweza kuleta athari ikiwamo uharibifu wa miundombinu na mali na makazi kuzunguukwa na maji.

Athari zingine zinazoweza kutokea  hatari kwa maisha ya watu kutokana na maji kutiririka kwa kasi, ucheleweshaji wa usafiri na kusimama kwa baadhi ya shughuli za kiuchumi.

Kwa upande wa tahadhali ya upepo mkali na mawimbi makubwa TMA imesema athari zinazoweza kujitokeza katika mikoa hiyo kuathirika kwa shughuli za uvuvi, ucheleweshaji wa usafiri pamoja na kuanguka kwa majani na matawi ya miti.

Kesho Alhamisi Januari 23, 2020 imesema mvua kubwa inatarajia kunyesha katika maeneo ya mikoa ya Lindi, Mtwara, Ruvuma na kusini mwa mkoa wa Morogoro.

Ijumaa ya Januari 24, 2020 mvua kubwa itanyesha kwa baadhi ya maeneo ya mikoa ya Lindi, Mtwara, Ruvuma na kusini mwa mkoa wa Morogoro.

TMA imesema Jumamosi ya Januari 25, 2020 mvua kubwa itanyesha kwa baadhi ya maeneo ya mikoa ya Lindi, Mtwara, Ruvuma.

Mamlaka hiyo imetoa tahadhari kwa wananchi wakati wa kipindi hicho kuhakikisha wanachukua hatua.