TMA yatangaza kupatwa kwa mwezi, kuonekana Tanzania

Thursday January 9 2020

 

By Baraka Samson. Mwananchi

Dar es Salaam. Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) imetangaza kutatokea tukio la kupatwa kwa mwezi kuanzia kesho Januari 10, 2020 saa 2:07 usiku hadi saa 6:17 usiku wa kuamkia Januari 11, 2020 na tukio hilo litaonekana sehemu yote ya Tanzania.

Taarifa iliyotolewa na TMA leo Alhamisi Januari 9, 2020 imeeleza kutokea kwa tukio hilo hakuna athari zozote kubwa zinazotarajiwa kutokana na hali hiyo.

Hata hivyo, mamlaka hiyo imeeleza upo uwezekano wa kuongezeka kwa kina cha maji katika bahari wakati maji kujaa, hali hii ikiwa inasababishwa na mvutano kati ya mwezi na maji katika bahari.

TMA imesema hali ya anga inatarajiwa kuwa yenye mawingu kidogo hali ambayo itatoa nafasi nzuri ya kuonekana kwa tukio hilo kwa macho.

Tukio hili hutokea au kujirudia mara chache sana katika eneo husika, hii ndio sababu kwa watu wa eneo husika na wanasayansi limekuwa ni tukio muhimu na la kipekee

Hali ya kupatwa kwa mwezi ni tukio la aina yake linatokea pale ambapo dunia inapita kati ya Jua na Mwezi, hivyo dunia husababisha kivuli katika uso wa mwezi. Muda wa kufunikwa kabisa ni dakika chache tu katika eneo husika.

Advertisement

Kupatwa kwa mwezi kunatokea wakati dunia, mwezi na jua vinapokaa kwenye mstari mmoja mnyoofu. Kutokana na hali hiyo kupatwa kwa mwezi kwa maeneo yaliyo mengi kunaonekana kwa watu wengi kama kupungua kwa mng’aro wa mwezi.

Wanasayansi wanaelezea kupatwa kwa mwezi kama tukio linalotokea na  huonekana katika namna tofauti tofauti mfano; ni kupatwa kwa mwezi kikamilifu (Umbra) hali ambayo huonekana pale hutokea giza katika uso wa mwezi hutokea kwa kipindi kifupi.

Aina ya pili ni kupatwa kwa mwezi kisehemu (Penumbra) hii hutokea wakati dunia inaposababisha kivuli hafifu katika uso wa mwezi.

Tukio la kupatwa kwa Januari 10 na 11, 2020 ni la kupatwa kwa mwezi kisehemu (Penumbra). Tukio hili litaonekana katika nusu ya Dunia hususan maeneo ambayo tarehe hii utakuwa usiku (Ulaya, Asia, Australia na Afr

Advertisement