TMA yatangaza mvua kubwa mikoa 20 Tanzania

Muktasari:

  • Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA)  imetoa tahadhali ya  mvua kubwa zinazotarajia kunyesha kwa siku mbili katika mikoa 20, Februari mosi na Februari 2, 2020.

Dar es Salaam. Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA)  imetoa tahadhali ya  mvua kubwa zinazotarajia kunyesha kwa siku mbili katika mikoa 20 nchini humo.

Mikoa hiyo ni Kagera, Geita, Shinyanga, Mwanza, Mara, Simiyu, Arusha, Manyara, Kilimanjaro, Kigoma, Tabora, Katavi, Rukwa ,Mbeya, Dodoma, Tanga ,Rukwa, Njombe, Iringa na Singida

Taarifa ya TMA iliyotolewa jana Jumatano Januari 29,2020 ilisema mvua hizo zitaanza kunyesha Februari Mosi hadi Februari 2, 2020 ambazo zinaweza kuleta athari ikiwamo uharibifu wa miundombinu na mali

Athari zingine  ni makazi kuzungukwa na maji, ucheleweshaji wa usafiri na kusimama kwa baadhi ya shughuli za kiuchumi na kijamii.

TMA imewataka wananchi kuchukua tahadhali na hatua stahiki hivyo waendelee kufuatilia taarifa za  hali hewa na itatoa mrejesho kila itakapobidi

Katika taarifa hiyo, TMA imeonyesha leo Alhamisi na kesho Ijumaa hakutakuwa na mvua maeneo yote nchini.