Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

TMA yatangaza mvua kubwa mikoa minne ikiwamo Dar

Muktasari:

Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) imetoa utabiri wa hali ya hewa kwa siku ya kesho Jumamosi ambapo mvua kubwa inatarajia kunyesha katika maeneo mbalimbali Tanzania Bara na Zanzibar.

Dar es Salaam. Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) imetoa tahadhari ya mvua kubwa inayotarajiwa kunyesha kesho Jumamosi 5, 2019 katika mikoa mbalimbali nchini ikiwemo Dar es Salaam.

Taarifa ya TMA iliyotolewa leo Ijumaa Oktoba 4, 2019 imeitaja mikoa mingine ni Pwani, Tanga, Zanzibar pamoja na kaskazini mwa mkoa wa Morogoro.

“Athari zinazoweza kujitokeza ni baadhi ya makazi kuzungukwa na maji, ucheleweshwaji wa usafiri, kusimama kwa muda kwa baadhi ya shughuli za kiuchumi na kijamii,” imeeleza taarifa hiyo