Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

'Mocha Mousse’ rangi ya mwaka 2025

Muktasari:

  • Pantone imekuwa na utaratibu wa kuteua rangi ya mwaka kwa zaidi ya miaka 25 sasa ambayo husaidia kuongoza watu katika shughuli mbalimbali haswa za masuala ya mitindo.

Dar es Salaam. Kila inapofika mwishoni mwa mwaka mamlaka ya kimataifa ya rangi - Pantone huchagua rangi ya mwaka unaofuata.

Kwa mwaka 2025 rangi ya 'Mocha Mousse' imechaguliwa kuwa rangi ya mwaka baada ya rangi ya Peach Fuzzy kutamba 2024.

Pantone imekuwa na utaratibu wa kuteua rangi ya mwaka kwa zaidi ya miaka 25 sasa ambayo husaidia kuongoza watu katika shughuli mbalimbali haswa za masuala ya mitindo.

                       

Kwa mujibu wa tovuti mbalimbali za mitindo zinaeleza kuwa ili kufikia uamuzi wa kuteua rangi fulani kuwa ndiyo rangi ya mwaka wataalamu kutoka Pantone hufanya uchunguzi kwa muda fulani juu athari za rangi duniani na katika tasnia mbalimbali kama vile mitindo, burudani, filamu, uchoraji, upambaji, maeneo ya kumbi za sherehe, michezo, maeneo maarufu ya kusafiri pamoja na hali ya kiuchumi kwa wakati huo.

Pia inaelezwa kuwa huzingatiwa teknolojia mpya zinazogunduliwa nyenzo, yanayoathiri rangi, mifumo husika ya mitandao ya kijamii na hata matukio yajayo ya michezo yanayovutia watu duniani kote. 

Inaelezwa kuwa uteuzi wa rangi huo unaofanyika kila mwaka imekuwa ina athari katika maamuzi ya mtu kununua vitu mbalimbali ikiwemo mavazi, vifaa vya majumbani, muundo wa picha, ufungaji na mambo mengineyo yanayohusisha rangi.


Mocha Mousse

Mocha Mousse kwa mujibu wa tovuti ya webflow ni moja kati ya rangi zinazotokana na rangi ya kahawia lakini yenyewe inataka kuelekea kuwa rangi ya ‘chocolate’ huku Pantone wakieleza kuwa rangi hiyo ipo katikati si rangi ya kuwaka sana wala si ya kupoa.

Inaeleza kuwa katika saikolojia ya rangi inaziainisha rangi hizo zilizotokana na rangi kahawia kuwa zinaashiria asili ya vitu katika mazingira.

                       

Kila mwaka rangi hizi hubeba ujumbe fulani kwa mwaka husika hivyo kwa mujibu wa tovuti ya Pantone rangi ya mwaka huu inahimiza utunzaji wa mazingira ya asili.

Kwa mujibu wa wataalamu wa masuala ya mitindo wanaeleza kuwa kuteuliwa kwa rangi fulani kuwa rangi ya mwaka kunasaidia watu kutotumia muda mrefu kutafuta rangi ambayo itatumika katika sherehe katika upande wa mavazi na mapambo.

Kauli hiyo inaungwa mkono na Magdalena Shao watu wanapokuwa na sherehe haswa kwa upande wa wanawake wamekuwa wakiumiza kichwa ni rangi ipi wanaweza kuvaa lakini inapoteuliwa rangi fulani kuwa rangi ya mwaka inakuwa msaada kwao na kuwasaidia kuendana na wakati.

Kwa upande wake Abduni Masud mkazi wa Kimara anasema masuala ya rangi ni ya wanawake kwa sababu huwa wana utaratibu wa kuwa na sare katika sherehe."Wanaume kwa asilimia kubwa hatunaga desturi ya kuwa na sare katika shughuli hivyo masuala ya rangi ya mwaka yanawahusu zaidi wanawake.

Naye, Mwanaisha Juma anasema yeye huwa anazingatia kupendeza zaidi kuliko suala la rangi ya mwaka.

Akizungumza na Mwananchi fundi wa nguo za kiume na kike kutoka Kilumbi Fashion, Abdul Kilumbi anasema rangi iliyoteuliwa mwaka huu ni nzuri na kama itavaliwa kwa kuchanganya na rangi nyingine ni vyema kuchagua rangi iliyopoa.