Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Diamond: Haji Manara hakupaswa kufungiwa na TFF hadi leo

Muktasari:

  • Diamond amesema yeye ni miongoni mwa watu ambao wanamfuatilia sana Haji, lakini kwenye sekeseke lake la kufungiwa hata kama aliteleza, alipaswa awe amefunguliwa muda mrefu, kutokana na mchango wake nchini kwenye upande wa mpira wa miguu.

Dar es Salaam. Nyota wa muziki nchini Diamond Platnumz ameshangazwa Haji Manara kuendelea kufungiwa na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), hadi leo.

Diamond amesema hayo alipokuwa akizungumza kwenye sherehe ya aliyekuwa msemaji wa klabu ya Yanga, Haji Manara ya kumbukizi ya siku yake ya kuzaliwa  na kumvisha pete mchumba wake Zaylissa.

Diamond amesema yeye ni miongoni mwa watu ambao wanamfuatilia sana Haji, lakini kwenye sekeseke lake la kufungiwa hata kama aliteleza, alipaswa awe amefunguliwa muda mrefu, kutokana na mchango wake nchini kwenye upande wa mpira wa miguu.

Mwaka 2022 kamati ya maadili ya TFF ilimfungia Manara miaka miwili kutojihusisha na masuala ya soka ndani na nje ya nchi na kulipa faini ya Sh20 milioni, kwa kosa la kumtolea maneno yasiyofaa Rais wa Shirikisho hilo,  Wallace Karia katika mechi ya fainali ya kombe la Azam iliyopigwa jijini Arusha.