Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Diddy kufanya ‘Party’ baada ya kutoka Gerezani

Muktasari:

  • Kwa mujibu wa taarifa zilizovuja kutoka katika Substack ya Rob Shuter, msanii huyo mwenye umri wa miaka 56 amepanga kufanya sherehe ya comeback itakayozidi zile za zamani za ‘White Parties’ alizokuwa akifanya miaka ya nyuma.

Marekani. Mkali wa Hip Hop kutoka Marekani ambaye kwa sasa anatumikia kifungo cha miaka minne gerezani, Sean Combs ‘Diddy’ amepanga kufanya sherehe ‘party’ kubwa baada ya kumaliza kifungo chake gerezani.

Kwa mujibu wa taarifa zilizovuja kutoka katika Substack ya Rob Shuter, msanii huyo mwenye umri wa miaka 56 amepanga kufanya sherehe ya comeback itakayozidi zile za zamani za ‘White Parties’ alizokuwa akifanya miaka ya nyuma.

“Kuna taarifa kwamba Diddy anataka kufanya sherehe kubwa zaidi ya kuachiwa kwake atakapotoka gerezani, inasemekena kuwa itakuwa sherehe kubwa kuliko zile alizokuwa akifanya nyumbani kwake. Anataka iwe kama sherehe ya kutawazwa kwa mfalme,” kimesema chanzo hicho.

Inaelezwa kuwa taarifa hiyo inakuja baada ya nyaraka mpya kutoka makahamani zikionesha tarehe ya kuachiwa kwa Diddy itakuwa Aprili 25, 2028 wakati hapo awali ilikuwa ni Juni 4, 2028.

Kwa sasa, rapa huyo ambaye amewahi kutamba na ngoma kama ‘All About the Benjamins’ anatumikia kifungo chake katika gereza la Fort Dix Federal Correctional Institution, lililopo New Jersey.

Licha ya tarehe hiyo ya kuachiwa kufahamika lakini kadri siku zinavyozidi kwenda tarehe ya kuachiwa kwake itakuwa karibu zaidi hii ni kutokana na ushiriki wake katika Programu ya Urekebishaji wa Matumizi ya Dawa za Kulevya (Residential Drug Abuse Program RDAP) ambapo anatajwa kushiriki kikamilifu.

“Anajikita katika mchakato wa mabadiliko na kwa kweli amepania sana kubadilika, anaamini kwamba kufungwa jela sio adhabu na badala yake kunamfanya awe bora kila siku,” imeeleza timu ya Diddy.

Kuhusu baadhi ya mashabiki wanaoamini kuwa staa huyo tayari ameshaondoka kwenye ramani ya burudani, kwa upande wake anaamini jamii itampokea tena kwa ukubwa. 

“Anaamini watu wengi duniani wanapenda sana kuona au kusikia stori za mtu maarufu anayepitia anguko au matatizo kisha baadaye anarudi tena kwenye mafanikio yake,” imeeleza timu ya staa huyo.


Mbali na kifungo hicho cha zaidi ya miaka minne, pia alihukumiwa miaka mitano ya uangalizi wa karibu (supervised release) baada ya kupatikana na hatia katika makosa mawili ya kusafirisha watu kwa lengo la ukahaba, ambayo yalimuhusisha aliyekuwa mpenzi wake Cassie Venture.

Hata hivyo, mahakama haikumtia hatiani katika mashtaka ya kula njama za uhalifu (racketeering conspiracy) na usafirishaji wa binadamu kwa ajili ya unyanyasaji wa kingono.


Ikumbukwe Diddy alikamatwa Septemba 16, 2024 kwenye moja ya hoteli jijini New York na alihukumiwa Oktoba 3, 2025.