Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Dongo la Alikiba kalitupa kwa Diamond?

WAKONGWE Pict

Muktasari:

  • Alikiba alitoa kauli hiyo katika show yake jijini Mwanza iliyofanyika hivi karibuni, hatua ambayo ni mwendelezo wa wasanii hao kutupiana vijembe katika nyimbo zao, majukwaa na hata mahojiano mbalimbali

Dar es Salaam. Supastaa wa Bongo Fleva kutoka Kings Music, Alikiba amegonga tena vichwa vya habari hasa mitandaoni baada ya kauli yake iliyotafsiriwa na wengi inamlenga hasimu wake kimuziki, Diamond Platnumz.

Alikiba alitoa kauli hiyo katika show yake jijini Mwanza iliyofanyika hivi karibuni, hatua ambayo ni mwendelezo wa wasanii hao kutupiana vijembe katika nyimbo zao, majukwaa na hata mahojiano mbalimbali.

"Kwa sasa watatoa ngoma zingine na zingine na zingine.... Halafu mimi nitatoa nyingine  moja...," alieleza Alikiba, mshindi wa tuzo ya MTV EMAs 2016.

Kauli ya Alikiba imekuja siku chache baada ya Diamond kuachia wimbo wake mpya, Joy (2026) akiwa na Jux, ukiwa ni wimbo wa nne kwa wawili hao kushirikiana.

Wimbo huo ulikuja kwa kushtukiza baada ya ule wa awali, Happy (2026) uliotoka takribani wiki mbili zilizopita, kupitwa views (idadi ya kutazamwa) YouTube na ule wa Bien na Alikiba, Finale (2026) unaofanya vizuri zaidi kwa sasa hasa huko Kenya.

WAKO 01

Hadi Jumanne ya wiki hii, video ya 'Happy' ilikuwa imetazamwa YouTube mara milioni 8.2 ndani ya wiki mbili (siku 14+), wakati 'Finale' ilikuwa na milioni 10.6 ndani ya siku 12 tu!, hivyo iliikuta na kuipita hiyo ya Diamond.

Hilo ndiyo hasa linaonekana kama sababu ya kumfanya Diamond kukimbilia kutoa hiyo kolabo yake na Jux ili kuuzima moto wa Alikiba na Bien. Na huu ndio hasa msingi wa kauli ya Alikiba katika show yake hiyo kuwa; Watatoa ngoma zingine na zingine na zingine.....!.

Hata hivyo, hii si mara ya kwanza kusikia kijembe kutoka kwa Alikiba kwenda kwa Diamond, pia Diamond naye amewahi kurusha vijembe vingi tu kwenda kwa Alikiba. Je, ni lini na kwa namna gani?, makala haya yanaenda kuangazia hilo kwa sehemu.

Katika wimbo wa Fid Q, Fresh Remix (2017) ambao Diamond pia alishirikishwa, alitumia verse yake kutupa vijembe kwa Alikiba akijitambulisha kama Simba kutoka mbuga ya Tandale ingawa suala wanalazimisha wawe sare sare!.

"Ukinichukia sikosi hela, hivyo kwangu sio case. Kuni-compare na Cinderella haiwezi kuwa fresh.... Viuno vidogo wanataka pensi ya pepе kale, Si walitaka kiti nimewapa hadi kitanda wakalale," anarap Diamond.

WAKO 02

Kwa mistari hiyo, Diamond hataki kushindanishwa na mtu aliyemtaja kama Cinderella, je, ni nani huyo?. Ikumbukwe Alikiba ana wimbo unaitwa Cinderella (2007) na ndio uliobeba jina la albamu yake ya kwanza, hivyo tunaweza kupata picha kijembe hicho ni cha nani hasa.

Pili, Diamond anasema 'walitaka kiti nimewapa hadi kitanda wakalale', hii inatukimbusha ujio mpya wa Alikiba baada ya mapumziko marefu na alisema amekuja kukalia tena kiti chake cha Ufalme wa Bongo Fleva na ndipo akaachia wimbo wake, Mwana (2014), hivyo kauli ya Diamond ilimlenga yeye pia.

Alikiba alikuja kujibu mapigo kupitia wimbo wake, Mediocre (2020) akijitambulisha kama mtoto wa Kariakoo ambaye kwake ushamba ni mwiko. Hapo alimjibu Diamond aliyesema yeye ni Simba kutoka mbuga ya Tandale ingawa swala wanalazimisha wafanane.

WAKO 03

"Njaa mimi nashiba, unaishi kwa kuniiga, and I'm alright. Ushamba mwiko kwa mtoto wa Kariakoo, Sichezi na dada zangu, nacheza na dada yako, mixer mkong'oto," aliimba Alikiba katika Mediocre (2020).

Utakumbuka Alikiba aliwahi kushirikiana na  dada wa Diamond, Queen Darleen katika wimbo, Najua Nakupenda (2006), na huu ndio pengine msingi wa mstari huo wa mwisho wa Alikiba.

Ukaribu wa Queen Darleen na Alikiba kwa kipindi cha nyuma ilipelekea watu kuhisi wawili hao ni wapenzi, lakini Darleen Januari 2017 alikanusha tena hilo katika mahojiano na EATV na kusema hakuna kingine kati yao zaidi ya urafiki.

“Alikiba alikuwa mshikaji wangu, yaani ni ndugu kabisa, hivyo watu waliona natoka naye kwa kuwa nilikuwa karibu naye, nazunguka naye mara kwa mara karibu sehemu zote, ila hajawahi kuwa mtu wangu," alisema Queen Darleen.

WAKO 04

Hata hivyo, Alikiba kupitia wimbo wake huo, Mediocre (2020) unaoaminika na wengi kuwa unamlenga Diamond kwa njia moja ya nyingine, ndipo anasema; Sichezi na dada zangu, nacheza dada yako.

Mapema Oktoba 2016, Alikiba alimtuhumu meneja wa Diamond, Sallam SK kwa kumfanyia figisu hadi kuzimiwa maiki katika tamasha la Mombasa Rocks Music huko Kenya.

Basi Diamond akatumia tukio hilo kurusha kijembe kwa Alikiba, ni kupitia wimbo wa Rich Mavoko, Kokoro (2016) ambao alishirikishwa ambapo mwishoni anasikika akisema "wamezima", akiwa na maana Alikiba kuzimiwa maiki.

Hivyo hili jipya la Alikiba, ni mwendelezo wa wasanii hao kurushiana tu vijembe na kwa namma moja imekuwa ikichangamsha muziki wao, na ndio kitu ambacho mashabiki wengi wanapenda mbali na kazi zao.