Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Dulla Makabila asaka mwanasaikolojia kisa Zaiylissa

Muktasari:

  • Akizungumza na Mwananchi, Dulla amesema kila anapokuwa peke yake humkumbuka Zaiylissa na wakati mwingine hujikuta akijilaumu kwa uamuzi alioufanya kwa hasira, jambo ambalo linamfanya ashindwe kuendelea na maisha yake kwa utulivu.

Dar es Salaam. Mwanamuziki wa Singeli, Dulla Makabila, amesema anatafuta msaada wa mwanasaikolojia ili kumsaidia kumsahau aliyekuwa mke wake, Zaiylissa, akieleza kuwa hadi sasa bado anasumbuliwa na kumbukumbu zake na hujuta kwa nini aliamua kumpa talaka.

Akizungumza na Mwananchi, Dulla amesema kila anapokuwa peke yake humkumbuka Zaiylissa na wakati mwingine hujikuta akijilaumu kwa uamuzi alioufanya kwa hasira, jambo ambalo linamfanya ashindwe kuendelea na maisha yake kwa utulivu.

"Natafuta mwanasaikolojia anisaidie nimsahau. Kila nikikaa peke yangu namkumbuka sana, na hata nikikutana naye sehemu yoyote nachanganyikiwa. Kuna wakati najutia kabisa kwa nini nilimpa talaka," amesema Dulla.


Kauli hiyo imekuja ikiwa ni muendelezo wa maungamo ambayo msanii huyo amekuwa akiyatoa mara kadhaa kuhusu kuvunjika kwa ndoa yake, ambapo awali aliwahi kukiri hadharani kwamba alifanya uamuzi wa kutoa talaka akiwa na hasira na baadaye akagundua alikuwa bado anampenda Zaiylissa. Pia aliwahi kusema huumia kila anapomuona au anapoona taarifa zinazomhusu akiwa na maisha yake mapya.

Dulla na Zaiylissa walifunga ndoa Mei 2023, ikadumu kwa takribani miezi mitatu kabla ya msanii huyo kuthibitisha kuwa ametoa talaka.

Tangu wakati huo, simulizi ya wawili hao imeendelea kuvuta hisia za mashabiki wa burudani kutokana na jinsi ilivyoanza kwa kishindo na kumalizika ndani ya muda mfupi.