Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Ferooz afichua walichogundua wanaume kwenye kikao chao cha mwisho

Muktasari:

  • Ferooz aliyewahi kutamba na nyimbo kali kama Mkiwa, Starehe, Kamanda, Bosi na nyinginezo ameliambia Mwananchi kuwa  mastaa wengi wa kiume wamegundua kwamba mapenzi ya kweli hayapo upande mmoja tu kwa mabinti, bali hata wao wanaume wanatakiwa kuwa kwenye mapenzi.

Dar es Salaam. Mwanamuziki mkongwe wa Bongofelva, Ferooz Mrisho maarufu kama Ferooz amedai wasanii wengi wa kiume wanataka mapenzi ya kweli kutoka kwa wanawake.

Ferooz aliyewahi kutamba na nyimbo kali kama Mkiwa, Starehe, Kamanda, Bosi na nyinginezo ameliambia Mwananchi kuwa  mastaa wengi wa kiume wamegundua kwamba mapenzi ya kweli hayapo upande mmoja tu kwa mabinti, bali hata wao wanaume wanatakiwa kuwa kwenye mapenzi.

Ingawa hakutaka kuingia kwa undani, mwanamuziki huyo alisema zamani wasanii wengi wa kiume walitumia fedha kuwarubuni mabinti, lakini sasa mambo yamebadilika kwani wasanii wengi wanaume wanataka mapenzi ya dhati kutoka mioyoni mwa wapenzi wao.

"Wasanii wengi wa kike wamekuwa wakitajwa kuwa na mahusiano na wanaume wenye pesa, ila mimi nasema kwa upande wa wasanii wa kiume wanawapenda wanawake kutoka moyoni," alisema Ferooz.

Pamoja na kauli ya mkongwe huyo kumekuwapo na hisia mbalimbali kuhusu mahusiano ya wasanii, ambapo baadhi ya watu wamekuwa wakidai kwamba mara nyingi hutumia fedha na umaarufu kuwarubuni mabinti ili kujihusisha nao kimapenzi.