Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

FID Q Amani ilileta pesa, pesa imeleta vita

FID 03

Muktasari:

  • Msanii wa Hip Hop Bongo, Fid Q ni mfano wa samaki majini ambaye hataki machozi yake yanayomtoka kuhusu jambo hilo kusombwa na maji, anatoka katika himaya yake hadi nchi kavu na kuzungumza.

Dar es Salaam. Kuna madai kwamba licha ya wasanii wengi kuwa na majina makubwa lakini wamekuwa wakiishi maisha ya kawaida sana, huku wengi wao wakiishi maisha ya mateso lakini wanashindwa kusema kutokana na kuteswa na kivuli cha umaarufu walionao mbele ya jamii.

Msanii wa Hip Hop Bongo, Fid Q ni mfano wa samaki majini ambaye hataki machozi yake yanayomtoka kuhusu jambo hilo kusombwa na maji, anatoka katika himaya yake hadi nchi kavu na kuzungumza.

“Bonge la staa, bonge la njaa hauna kitu, jikombe ugongwe mtaaa ukuone hauna ishu, ukishindwa kujiandaa jiandae kushindwa,” Fid Q anasema katika wimbo wake ‘Siri ya Mchezo’ aliyomshirikisha Juma Nature.

Kitendo cha kutoka kwenye himaya yake na kuzungumza ni ujasiri alionao Fid Q pekee yake hadi samaki wengine wanashangaa ila ni uwezo tu aliojaliwa ili kuiponya jamii yake.

“Wanapagawa na baadhi ya mambo ninayoyajua, pia nina uwezo wa kufanya mpaka madawa yanaugua,” anasema tena Fid Q katika wimbo huo uliomuwezesha kushinda tuzo mbili za muziki Tanzania (TMA) 2014.

FID 01

Kushinda tuzo hizo kulimfanya kufikisha tuzo nne za TMA ukijumlisha ile ya mwaka 2006 kupitia wimbo, Mwanza, pia aliyoshinda mwaka 2007 kupitia wimbo ‘Ni Hayo Tu’ aliomshirikisha Professor Jay na Mmarehemu Langa.

Agosti 13 ndio tarehe aliyozaliwa, ndiye msanii mwenye birthday kubwa zaidi Bongo kutokana na ukubwa wa wimbo wake, August 13 (2006) ambao ameeleza mapambano ya maisha yake hadi kuwa Fid Q wa leo, ni mapito ambayo wengi wetu tunayapitia.

Mwanzoni kabisa (intro) Salama Jabir anamuelezea Fid Q ni nani hasa, kubwa zaidi ni maisha ya kulelewa na Bibi yake kwa sababu mama yake alikuwa anafanya kazi, hiyo ni baada ya baba yake kuondoka nyumbani na kwenda kuanzisha familia nyingine!

“Dingi haonekani nyumbani majukumu yote mama yangu, nimeona nimejifunza mengi kwa kujiongeza kivyangu,” anasema Fid Q katika wimbo huo, kisa cha kutoishi na baba yake kakizungumzia tena kwenye wimbo wake, Faith.

“Sikutaka kujua baba ni mtu wa aina gani, ila nilitaka anishike mkono ili niweze kua, nisishinde mtaani ndoto ambayo haijawahi kuwa,” Fid Q anaeleza kwa hisia.

FID 02

Utafutaji wa maisha anaweza kutajwa kuchochea wazazi wengi kuwa mbali na familia zao, hizi ni ‘Juhudi za Wasiojiweza’ ambao ni wimbo wa Fid Q aliomshirikisha marehemu Bi Kidude, unapatikana katika albamu yake ya tatu, Propaganda (2009). 

“Amani ilileta pesa, pesa imeleta vita” anachana Fid Q akiwa na maana kuwa uwepo wa amani duniani ndio uliochochea uwepo wa shughuli nyingi za uzalishaji, ila uhitaji mkubwa wa rasilimali katika uzalisha umeleta vita na kuathiri familia nyingi.

Katika wimbo wake ‘Ripoti za Mtaani’ akimshirikisha Zahir Zorro, Fid Q ameelezea maisha ya binti ambaye alilazimishwa kuolewa na wazazi wake kwa sababu aliyekuwa akitaka kumuoa alikuwa na uwezo mkubwa kifedha.

“Siku zikapita akaanza kufeli, kwa kuwa uongo aliuzidisha akajikuta yupo nje ya ukweli” anasema Fid Q baada ya yule binti kushindwa kuishi vizuri katika ndoa kitu kilichochangia mume kunywa sumu na kufariki.

Pengine hii ndio maana halisi ya ule mstari wake, ‘Amani ilileta pesa, pesa imeleta vita’.

FID 03

“Alipenda kwenda na tarehe akasahau siku huwa hazilingani, pesa huja na sterehe na matatizo humo humo ndani. Hakuna kinachokauka mapema zaidi ya machozi, japo macho hubaki mekundu na usoni ishara ya majonzi,” anasema Fid Q katika wimbo huo.

Hata hivyo, baadaye binti alikuja kupata mume mwingine lakini pia hawakudumu kutokana na tabia zake, ndipo Fid Q anamaliza kwa kusema; “Si wote aliowavisha kofia walikuwa na vichwa, hakuhesabu alichopoteza bali alichobakiza”.

Hiyo ina maana licha ya binti kumpoteza mume wake na hata wanaume wengine aliokuja kukutana nao hapo baadaye, bado hakutaka kujiua kama mume wake wa awali, alithamini uhai wake kwani ndicho pekee alichobakiza maishani. 

Rapa huyu anakiri kuwa uwezo wake wa kuandika mashairi unatokana na tabia aliyojijengea ya kujisomea sana vitabu kitu ambacho kimemjenga na ndilo chimbuko la albamu yake ya tatu.

Kwa ujumla tayari Fid Q ametoa albamu nne, Vina Mwanzo Kati Na Mwisho (2005), Propaganda (2009), KitaaOLOJIA (2019) na KitaaREJEX (2025) ambayo imejumuisha nyimbo zilizokosa nafasi katika KitaaOLOJIA.

Ikumbukwe Hardmad ndiye mtu wa kwanza kumpeleka Fid Q pale MJ Records kwa Master J aliporekodi wimbo wake ‘Huyu na Yule’ akimshirikisha Mr. Paul, wimbo huo ulimtambulisha vizuri ndani ya Bongofleva kama rapa tishio.