Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Jay Melody amng'ata sikio Clemant Mzize

Muktasari:

  • Katika mazungumzo yake na Mwananchi, Jay Melody amesema hapa nchini anazipenda Simba na Yanga kutokana na watu, lakini mbali na hilo hajawahi kujua yupo upande gani kama ilivyo kwa watu.

Dar es Salaam. Msemo wa wahenga wa Mungu hakupi vyote, unaishi kwa msanii wa kizazi kipya, Jay Melody. Licha ya sauti nyororo aliyonayo, lakini akikusimulia kuhusiana na mpira wa miguu utacheka mpaka basi!.

Katika mazungumzo yake na Mwananchi, Jay Melody amesema hapa nchini anazipenda Simba na Yanga kutokana na watu, lakini mbali na hilo hajawahi kujua yupo upande gani kama ilivyo kwa watu.

"Nakumbuka utotoni tulikuwa tukicheza mpira wa visoda, basi mimi nilikuwa nakusanya vya timu ya Manchester ninayopenda hadi sasa ila za hapa nyumbani sikuwahi kufanya hivyo," amesema Jay Melody na kuongeza:

"Mfano kuna kipindi nilikuwa naipenda Simba kwa sababu ya Haji Manara akiwa msemaji wa timu hiyo, nikajikuta naipenda Yanga kwa sababu ya Fiston Mayele akifanya vizuri. Zinapokutana Simba na Yanga inayoshinda ndiyo ninayoiunga mkono, mfano nikikaa kijiweni wingi wa watu kuishabikia timu fulani naungana nao, yaani mimi katika mpira ni shabiki ambaye nipo nipo tu, sinaga machungu kama wengine ambao hawadi wanalia, wanakosa furaha."

Mbali na hilo, amesema msemaji wa timu anayempenda kwa sasa ni Ahmed Ally wa Simba kwa namna anavyopangilia maneno kwa vina, na kwamba humuona kama anarapu au kuimba.

"Jamaa kwanza ni kama msanii kwa namna anavyoongea kwa kupangilia maneno, hana hasira licha ya timu yake kutochukua ubingwa bado anatoka mbele ya watu kuitetea timu, akiongea lazima utacheka," amesema msanii huyo na kuongeza:

"Ila ninachokipenda wakikutana na msemaji wa Yanga, Ally Kamwe, utadhani wapo timu moja. Hicho ni kitu kizuri kinaonyesha mpira siyo vita, wachezaji ninaowapenda kwa sasa ni Clemant Mzize nimshauri pesa zinazotajwa kwake za usajili asiziache sisi wote ni vijana tunapambana kujenga maisha yetu kiuchumi, ingawa sijui taratibu zinakuaje, ninachoamini ana akili kubwa ya kufanya maamuzi ya manufaa kwake."