Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Jiongeze: Binti'z wa mastaa watatu wenye majina ya Joseph

Muktasari:

  • Ukirudi nyumbani Bongo pia kuna Profesa Jay. Ni staa mkubwa sana wa muziki wa kizazi kipya kutoka ardhi ya Nyerere. Ni miongoni mwa nyota wa awali walioleta mapinduzi makubwa ya muziki wetu

Dar es Salaam, Ukienda Uganda, kwa wanamuziki wa kizazi cha milenia mpya. Bila shaka utaanza kutajiwa jina la Jose Chamilione. Nyota kutoka kwenye ardhi ya Yoweri Kaguta Museveni. Jamaa ni staa wa kitambo.

Ukirudi nyumbani Bongo pia kuna Profesa Jay. Ni staa mkubwa sana wa muziki wa kizazi kipya kutoka ardhi ya Nyerere. Ni miongoni mwa nyota wa awali walioleta mapinduzi makubwa ya muziki wetu.

Na kuna Sugu. Huyu alikuwa ndiye taa ya muelekeo wa dili la muziki Bongo. Mwanzoni mwa miaka ya 90, akawa staa mkubwa sana wa muziki wa ‘rap’. Katikati ya dansi, taarabu na kama siyo mduara naye akachomoza.

Ajabu la kwanza. Jose Chamilione uzao wake wa kwanza ni wa kike mtoto aitwaye Anna. Prof. Jay uzao wake wa kwanza ni wa kike, mtoto aitwaye Lissa. Sugu pia uzao wake wa kwanza ni wa kike, mtoto aitwaye Sasha.

Kama haitoshi endelea kujiongeza hapa. Ajabu lingine toka kwa nyota hawa wa muziki Afrika Mashariki. Ni kwamba majina yao ya ubatizo wote ni Joseph. Ni Joseph Haule, Joseph Mayanja na Joseph Mbilinyi. 

Na kimsingi mbali na kufanana kwao kwa uzao wao wa kwanza. Pia kufanana kwao dhehebu la dini yaani Wakatoliki.

Baba Lissa, Baba Anna na Baba Sasha. Tazama hata majina ya watoto wao ni mafupi yote. Mungu kawa jalia watoto wa kike na Mungu ukiomba mkate hakupi jiwe.

Mtume Mohamed naye alisema ukimsomesha mtoto wa kike, ujue umesomesha jamii nzima na ndicho wanachofanyiwa watoto hawa na wazazi wao, Mungu awalinde.

Tuishi!