Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Jiongeze: Tofauti ya Ngwea na Hawa

Muktasari:

  • Ngwea alikuwa sanaa na sanaa ilikuwa Ngwea. Watu sampuli ya Ngwea huzaliwa mara chache. Hawazaliwi kila mara kama fundi viatu, simu, saa na umeme. So, unapaswa uwe sehemu ya jamii iliyoishi pale Ngwea akiwa top top. Usijilishe upepo leo.

Dar es Salaam. Kuna ‘Gen Z’ hujiaminisha kuwa ni wakali zaidi ya Ngwea. Kwenye mitindo huru (freestyle), bahati mbaya zaidi wanahojiwa na watu waliokuwa ‘auti ofu richi’, kipindi ‘Albatinyo’ yupo kwa ‘praim’ yake. Oya! Lile lilikuwa jini wazee kaa mbali. 

Ngwea alikuwa sanaa na sanaa ilikuwa Ngwea. Watu sampuli ya Ngwea huzaliwa mara chache. Hawazaliwi kila mara kama fundi viatu, simu, saa na umeme. So, unapaswa uwe sehemu ya jamii iliyoishi pale Ngwea akiwa top top. Usijilishe upepo leo.

Kama ulikuwa Muheza unasikia tu Ngwea Ngwea. Ama ulikuwa Tanangozi na Mtwivira unapata simulizi tu za Ngwea. Ni rahisi kuaminishwa na wapiga kelele kuwa wanaweza zaidi ya Ngwea. Utapiga mbizi kwenye lami mzee na usipate wa kukuokoa.

Ngwea hakuwa hafanyi ‘friistaili’ kuunganisha maneno mfanano tu. Ngwea aligonga ‘friistaili’ na ladha ndani yake. Ana ‘frii staili’ kiufundi huku akinata na mdundo ‘kiswaga’. Alikuwa kama mvivu hivi akiwa anachana, lakini anaua na mdundo wowote ule. 

Ngoma zake kadhaa ni zao la mitindo huru. “Napokea Simu” chanzo ni ‘kufrii staili’ ngoma ya “Promota Anabeep” ya Pro. Jay, Singida Dodoma, Geto Langu nk. Alichofanya ni kwenda studio kuuboresha kwa kuongeza kitu au kusakafia ili liwe pini kamili. 

Madogo wanaopiga mitindo huru kwa sasa siyo wabaya. Ubaya ni kujitanua kwa Ngwea. Hawa siyo ‘klasi’ ya Albato, ufundi na ladha hawana. ‘Wanafloo’ kimifanano. Yeye ‘alifrii staili’ na minato iliyokufanya ujitikise bila kutaka. Fundi kweli.

Ngwea ndo bishoo aliyekubalika na wahuni kuliko mabishoo. Ndo msanii ambaye alifunika kwenye shoo kubwa kwa ‘frii staili’ bila hata kugonga mipini yake. Yeye ‘zilihiti’ ngoma zake na vesi zake katika ngoma za wenzake. Yule ni GOAT kweli wala siyo utani.

‘Alifrii staili’ bar, ‘alifrii staili’ studio, ‘alifrii staili’ ‘stejini’ ‘alifrii staili’ kwenye ‘intavyuuzi’ radio. Na kote angekupa ladha tofauti kwa sababu hakutunga kabla. Alipiga mistari ya papo kwa papo kulingana na mazingira. Anakupa kitu kinachokuzunguka ulipo.

Kama umamuheshimu Prof. Jay, Fid Q, Mwana FA, Sugu, Jaymoe, Diamond, Lady Jaydee na wote. Basi hao wote walimuheshimu sana Ngwea. Na walikiheshimu sana kipaji cha Ngwea. Hata wao wanasema hakuwahi kutokea na hajatokea. ‘Jiheshimuni kidogo’.