Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Jiongeze: Unataka Zuchu aolewe 

Muktasari:

  • Wanachofanya ni kuhama hama tu na maneno yao. Leo wanataka f’lani azae. Kesho watataka flani aachane na flani. Keshokutwa watataka f’lani awe na f’lani na leo wanataka Zuchu alazimishe ndoa.

Dar es Salaam, Yes! Wabongo wanapenda kujipa umuhimu katika maisha ya watu. Wapo wanaoshangaa Bibie Zuchu ‘kudeti’ na Mondi bila ndoa. Yaani wanaoshangaa utadhani wao wana ndoa vile. Nongwa tu.

Wanachofanya ni kuhama hama tu na maneno yao. Leo wanataka f’lani azae. Kesho watataka flani aachane na flani. Keshokutwa watataka f’lani awe na f’lani na leo wanataka Zuchu alazimishe ndoa.

Ndoa nyingi zina migogoro kwa ‘ishu’ za kukurupuka. Papara bila kufahamiana vizuri. Kuna vitu vya msingi tunapaswa kufanya lakini tunapuuza. Ujuaji mwingi na kuishi kimazoea.

Huwezi kuanzisha uhusiano bila upendo wa dhati. Watu wanaoa au kuolewa baada ya kukutana baa au kampani tu. Akili na matamanio ya tungi yakupe mtu wa kuanzisha naye familia kweli?

Hujamchunguza nidhamu yake, adabu, hasira, ulevi au ukicheche. Hamjapeana ‘taimu’ kufahamiana, hata kujua kama ile rangi ni yake ya asili kweli au ni ‘Medi ini China’. We unakurupuka tu.

Lazima muwe kitu kimoja kabla ya kuwa mwili mmoja. Jichanganyeni maeneo tofauti kama michezoni, baa, sinema na out mbalimbali. Mjue ‘interesti’ za kila mmoja. Ili mshibane hata kwa imani tofauti.

Wajue ndugu zake, pata habari zao. Hizo zitafanya umjue mwenzako yukoje. Kama ana tabia mbovu mpotezee. ‘Ishu’ za kutegemea atabadilika ndani ya ndoa ziliponza wengi. Abadilike uchumbani siyo ndoa. 

Kimini, kipini, wanja, kope, kijora, sauti ya puani, kurembua macho, kutingisha wezere ndo kukupe mke? Utakuwa lofa. Six Packs, bia, urefu, kiduku, kununuliwa bando ndo awe mume? Utakuwa taahira. 

Wengi ‘wanadeti’ kwa miaka bila ndoa. Kwa sababu hawafai kuoana. Siyo kila uhusiano ufikie ndoa. Na siyo kila ndoa ianze kwa uhusiano. Ndoa ni ziadi ya vile urembo na pesa.