Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kabla ya Wema na Uwoya, hebu jitazame…

Kitaa ndoa nyingi zina migogoro kwa ‘ishu’ za kukurupuka. Kufanya papara bila kufahamiana vizuri. Kuna vitu vya msingi watu tunapaswa kufanya lakini tunavipuuza. Ujuaji mwingi na kuishi kimazoea au hisia za kipombe pombe tu.

Huwezi kuanzisha uhusiano bila kuwepo kwa upendo wa dhati. Watu wanaoa au kuolewa baada ya kukutana baa na kupendezwa na kampani tu. Yaani akili na matamanio ya tungi yakupe mume au mke wa kuanzisha familia?

Hujachunguza tabia kama ana nidhamu, adabu, hasira, mlevi au kicheche. Hamjapeana muda wa kutosha siyo tu kufahamiana, bali hata kujua kama ile rangi ni yake ya asili kweli au ‘Medi ini China’. Unakurupuka tu.

Lazima muwe kitu kimoja kwanza kabla ya kuwa mwili mmoja. Jichanganyeni maeneo tofauti kama michezoni, baa, sinema na out mbalimbali. Kujua ‘interesti’ za kila mmoja. Ili muwe mmeshibana hata wa imani tofauti.

Wajue ndugu zake, pata habari zao ambazo zitafanya ujue mwenzako yukoje. Kama ana tabia mbovu mpotezee. ‘Ishu’ za kutegemea atabadilika ziliwaponza wengi. Abadilike mkiwa wachumba siyo kwenye ndoa.

Dunia sasa inampa mwanamke ‘ova pawa’ hata akiwa kakosea. Malezi ya binti hufanya aamini kila kosa husababisha mwanamume. Huwafanya bintizi wazingue kusudi, wakijua jamii itasimama nao. Hili litazame kwa jicho la tatu.

Atatetewa na jamii yote. Kuanzia wanaume wenzako, Serikali mpaka mifugo ikibidi.

Kifupi miaka ya sasa wanaume hatuna chetu, ingawa ukweli unauma lakini huna jinsi zaidi ya kukubali ili uwe huru.

Ukiwa na misimamo binafsi bila kushirikisha yeyote. Imekula kwako. Dunia hii hata kupeleka kesi kwa wazee au mahakamani na wife akitoa boko basi atakutwa na hatia.

No! Hii ya sasa ‘wasiponyutolaizi’ kesi basi utageuziwa kibao.

Dunia iko na mwanamke ‘nau deizi’, kidume utaambiwa humridhishi, humtunzi, sijui hauko romantiki. Mashtaka yote ni kwako kama wewe ndio mkosaji, huku ‘waifu’ kazi yake kuongeza chumvi. Na wewe unabaki kusema haa!

Kumbe hapo ungerahisisha kwa kumfukuzia kwao bila hata kutaka vikao na wazazi. Sijui ushauri wa nani na nani wale ndezi wanaojifanya wao ndio wako ‘klini’. Achana na hekima za miaka ya 90 utaishia kujizolea dhihaka, kebehi na aibu kama hizi.

Acha kujibebesha matatizo yasiyokuhusu kwa kudhani ndio uwanaume. Kuzaliwa kidume raha sana, kinachotuponza ni sifa za kibwege. Tuna viherehere vya kubeba matatizo yasiyo yetu ili tusifiwe tu. Sisi ni ‘mapedeshee’ toka tumboni mwa mama zetu.

Chukua kalamu na karatasi, anza kuandika shida zote zinazokusumbua, kisha zichambue, lazima asilimia 90 kwenda juu sio umebebelea shida za wengine tu, kifupi tuna ujinga mwingi sana.

Fanya vitu unavyopenda, tunga sheria zako za kuendesha familia.

Achana na akili za kitumwa kutaka kujua ‘totozi’ inataka au kupendelea nini. Ndio maana kila siku vijana wa kiume hufungua komeo za kuumizwa tu, yote kutaka ‘kushea’ miamala na mwanamke.

Dunia ya sasa hata watoto wako wapo pamoja na ‘waifu’. Weka akiba yako mwenyewe, hapa kuwa na ubinafsi kiasi, hili utakumbuka siku ukiwa kwenye gofu lako peke yako. Na ‘waifu’ akiwa kwa watoto wako wamekutelekeza kiaina

Acha kujifanya dhaifu na mnyonge ukizani utapendwa na kuheshimiwa. Kidume sio dhaifu kwa ‘waifu’ kama wengi wanavyofikiri. Tatizo letu tunapenda kuvaa udhaifu ili tuziridhishe nyoyo za ‘mawaifu’.

Kwa watu dhaifu utasikia siku hizi mapenzi ya kweli hakuna. Hii ni kwa kuwa mfumo wa ‘laifu’ na tabia za watu zimekuwa kama za wanyama. Waliotuambiwa tulitokana na ‘nyani’ walikosea. Ila tunaelekea kuwa ‘manyani’. Watu hawajali kabisa kuhusu maana ya kupendana. Pita mtaani utaona mtoto wa kike analalamika kuwa siku hizi hakuna mapenzi ya kweli. Unajiuliza zamani aliiona wapi?

Kama anajua hakuna mapenzi ya kweli na yeye hana mpenzi. Kama anajua hakuna mapenzi ya kweli, lakini na yeye ana mpenzi, pia anakuwa sehemu ya tatizo.

Ndoa hazidumu kwa sababu kabla ya kufunga ndoa, watu huzingatia tukio la siku ya harusi kuliko maisha ya ndoa baada ya harusi. Bila kujua ndoa inaenda mbali zaidi. Kuna maisha ya ndoa na kuna tukio la harusi.

Wengi hupenda zaidi harusi. Huwaza ndoa katika taswira ya suti kali, shela toka Thailand. ‘Mekapu’ ya bibi harusi kutoka Zazie Masaki. Ile time ya mashosti kuingia ukumbini na wimbo wa ‘Alingo’. Kukomesha wanafiki jinsi sherehe itakavyokuwa.

Hawawazi mume au mke akiumwa miaka mitatu mfululizo utavumilia? Wakikosa watoto miaka mitano ya ndoa watahimili maneno ya ndugu wa mume? Mawifi na maneno ya kujaza choo cha kaka yao na huna kizazi?

Ndoa ni zaidi ya sherehe ya harusi. Baada ya yale matarumbeta kuzimika, usiku kifuatacho ni majukumu mazito na kiapo kisichovunjika. Acha mizuka ya Kwaito. Nenda mbali kidoogo. Uko tayari kuwa mume au mke wa mtu mmoja?

Mizuka ya ‘eksi’ utaweza kuikwepa kweli wewe? Huwa mnawaza hayo au zawadi ya kamati kutoa ‘Harrier Kalio la Nyani’? Kabla ya kuoa au kuolewa jiulize, unataka ndoa kweli au unataka mizuka ya sherehe ya harusi?

Ukisoma mitandaoni, stori za kitaa na ‘vipeji’ vya umbea.

Utawahukumu mastaa wetu hawa. ‘Coz’ tunajengewa picha kama wao ndio wenye ‘misteki’ kinoma kwenye idara ya uhusiano. Tusiwe wepesi wa kuhukumu.

Ukweli ni kwamba mitaani nako maseke ni mengi. Mastaa ni sehemu ya jamii yetu. Vitu wanavyofanya havitoki dunia nyingine.

Ni yaleyale yanachofanywa na jamii yetu. Na hili zaidi lipo kwenye ishu za ‘malavidavi’, kuna shida nyingi sana kama jamii.

Kinachotokea ni kwamba asilimia kubwa mambo yao yapo gizani. Lakini mastaa mambo yao yapo mwangani.

Yanaonekana kirahisi zaidi, wakati wanachofanya ni ‘pati tu ya gazeti’ ila huku mitaani. Ni shida.