Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kesi zaendelea kumuandama Diddy

Muktasari:

  • Diddy alihukumiwa Oktoba 2025, baada ya kukutwa na tuhuma nzito lakini alihukumiwa kwa makosa mawili ya biashara ya ngono (sex trafficking) na uhalifu wa kimtandao (racketeering).

Marekani. Wakati akiwa bado anatumikia adhabu ya miezi 50 ya kifungo jela, rapa na mfanyabiashara mkubwa wa muziki Marekani, Sean Combs 'P Diddy' huenda akaendelea kusalia gerezani kutokana na msururu wa kesi unaoendelea kutolewa dhidi yake.

Diddy alihukumiwa Oktoba 2025, baada ya kukutwa na tuhuma nzito lakini alihukumiwa kwa makosa mawili ya biashara ya ngono (sex trafficking) na uhalifu wa kimtandao (racketeering).

Taarifa kutoka Marekani zinaeleza Ofisi ya Mwendesha Mashtaka wa Wilaya ya Los Angeles imeanza kupitia madai mapya ya unyanyasaji wa kingono yaliyowasilishwa dhidi ya Diddy, hatua ambayo inaweza kuzaa mashtaka mapya ya jinai dhidi yake.

Kwa mujibu wa taarifa hizo, wachunguzi wanakusanya ushahidi na kupitia maelezo ya mlalamikaji ili kubaini kama kuna msingi wa kufungua kesi rasmi mahakamani.

Iwapo ushahidi utathibitisha madai hayo, Diddy anaweza kujikuta akikabiliwa na mashtaka mengine wakati tayari anaendelea kupambana na tuhuma kadhaa zinazohusiana na ukatili, biashara haramu ya ngono na makosa mengine mazito.

Kwa zaidi ya miaka 30, Diddy amekuwa miongoni mwa wasanii wenye ushawishi mkubwa katika muziki wa hip hop duniani.


Alianzisha kampuni ya Bad Boy Records iliyowatengeneza mastaa kadhaa wakubwa akiwemo The Notorious B.I.G., huku pia akijitengezea utajiri mkubwa kutokana na muziki, biashara ya mavazi, vinywaji na uwekezaji mwingine.

Lakini kuanzia mwishoni mwa mwaka 2023, taswira yake ilianza kuingia doa baada ya Cassie Ventura aliyewahi kuwa mpenzi wake kufungua kesi iliyofichua madai mazito dhidi yake.

Tangu wakati huo wanawake kadhaa wamejitokeza na kutoa madai yanayofanana, huku mamlaka za Marekani zikianza kufanya uchunguzi wa kina kuhusu mwenendo wake.

Miongoni mwa matukio yaliyotikisa zaidi ni kuvuja kwa video ya mwaka 2016 iliyomwonyesha Diddy akimpiga Cassie ndani ya hoteli moja jijini Los Angeles, jambo lililoibua hasira kubwa kutoka kwa mashabiki na wadau wa burudani duniani.

Licha ya changamoto hizo zote, Diddy ameendelea kusisitiza hana hatia na tuhuma nyingi zinazomkabili ni za kupangwa kwa lengo la kuchafua jina lake.

Hata hivyo, uchunguzi huu mpya wa Los Angeles unaonekana kuongeza presha mpya kwa rapa huyo ambaye kwa sasa anakabiliwa na moja ya nyakati ngumu zaidi katika maisha na historia yake ya muziki.