Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

King Kikii wa ‘Kitambaa cheupe’ afariki dunia

Mwanamuziki mkongwe wa muziki wa dansi Tanzania, Boniface Kikumbi maarufu King Kikii enzi za uhai wake

Muktasari:

  • Taarifa za kifo cha King Kikii zimethibitishwa na Katibu Mkuu Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo, Gerson Msigwa

Dar es Salaam. Mwanamuziki mkongwe wa muziki wa dansi Tanzania, Boniface Kikumbi maarufu King Kikii amefariki dunia usiku wa kuamkia leo Ijumaa Novemba 15, 2024.

Taarifa za kifo cha King Kikii zimethibitishwa na Katibu Mkuu Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo, Gerson Msigwa asubuhi ya leo kupitia ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa Instagram.

“Lala salama mzee wetu Boniface Kikumbi Mwanza Mpango (King Kikii), mwanamuziki mkongwe, jabali la rhumba na mtu mwenye utumishi uliotukuka katika tasnia ya muziki Tanzania.

“Tutauenzi mchango wako mkubwa katika muziki wa dansi Tanzania. Kwa miaka mingi umeburudisha, umefundisha, umeelimisha na uliipenda sana Tanzania,” ameandika Msigwa.

Enzi za uhai wake, King Kikiii alitamba na vibao mbalimbali kikiwemo maarufu cha ‘Kitambaa cheupe’.

Endelea kufuatilia taarifa zaidi katika mitandao yetu ya kijamii