Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Leo tena sherehe, harusi ya Jux, Priscilla

Muktasari:

  • Sherehe hiyo inayofanyika katika ukumbi wa The Superdome, Masaki inakuwa ya tatu ya harusi kwa wanandoa hao, ambao rasmi walifunga Februari 7, 2025 Mbezi Beach, Dar es Salaam.

Dar es Salaam. Moja kati ya tukio linalosubiriwa kwa hamu leo Mei 28, 2025, ni sherehe ya tatu ya harusi ya msanii wa Bongo Fleva, Juma Jux na mkewe kutoka Nigeria, Priscilla Ojo. 

Sherehe hiyo inayofanyika katika ukumbi wa The Superdome, Masaki inakuwa ya tatu ya harusi kwa wanandoa hao, ambao rasmi walifunga Februari 7, 2025 Mbezi Beach, Dar es Salaam.

Ndoa ambayo ilihudhuriwa na mastaa mbali nchini akiwemo Diamond Platnumz, Marioo, Abba Process, S2kizzy na wengine wengi.

Hata hivyo baada ya harusi hiyo Jux na familia yake walielekea nchini Nigeria kwa ajili ya harusi ya kitamaduni iliyofanyika Aprili 17, 2025. Ambapo msanii huyo alisindikizwa na mastaa akiwemo Diamond Platnumz, Ommy Dimpoz, Posh Queen, Korede Bello, Jimmy Chansa, Peter wa Psquare na wengineo.

Baada ya harusi hiyo Aprili 19, 2025, Jux na Priscilla walifanya sherehe nyingine ya harusi White Wedding ambapo wawili hao walifunga tena ndoa ya Kikristo ikiwa kama sehemu ya kuthamini dini ya mke wake Priscilla.

Harusi hizo zimefanya msanii huyo wa Bongo Fleva kujitanua kimuziki ukanda huo wa Magharibi mwa Afrika na kupelekea muziki wake kuendelea kufanya vizuri kwenye chati za muziki nchini Nigeria.

Utakumbuka, Jux na Priscilla walikutana kwa mara ya kwanza nchini Rwanda mwaka jana na kuanza mahusiano Agosti 2024, wawili hao walionekana kwa mara ya kwanza wakiwa pamoja kwenye moja ya kumbi za starehe jijini Dar es Salaam. Huku penzi lao likishamiri na kuteka mitandao ya kijamii ndani na nje ya Tanzania baada ya Jux kwenda ukweni nchini Nigeria.

Kwasasa Jux anatamba na Ep yake ' A Day To Remember' ambayo imebeba nyimbo saba za mapenzi ambazo ni God Design, Alolo, EX Wa Nani, Si Mimi, My Shayla, Celebration, na You. ambapo kwa mujibu wa Jux anakwambia Ep hiyo imebeba ujumbe kuhusu maisha yake ya ndoa.