Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Ma-dj ni hawa tu

Muktasari:

  • Katika taarifa hiyo, BASATA imekumbusha kuwa usajili na umiliki wa kibali halali ni takwa la kisheria kwa mtu yeyote anayejihusisha na shughuli za sanaa nchini.

Dar es Salaam. Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) limetoa orodha ya Manju Muziki (DJ's) waliosajiliwa rasmi na wenye vibali hai vya kufanya shughuli za sanaa nchini, huku likitoa wito kwa wadau wa burudani kuhakikisha wanawatumia DJ waliokidhi matakwa ya kisheria.

Katika taarifa hiyo, BASATA imekumbusha kuwa usajili na umiliki wa kibali halali ni takwa la kisheria kwa mtu yeyote anayejihusisha na shughuli za sanaa nchini.

“Kwa mujibu wa Kanuni ya 16 (1) (a) na (b) ya Kanuni za Baraza la Sanaa la Taifa za Mwaka 2026 inatoa mamlaka kwa Baraza la Sanaa la Taifa kurasimisha Wasanii na Wadau wa Sanaa pamoja na kutoa vibali vya shughuli zote za sanaa nchini.


“Aidha, Baraza la Sanaa la Taifa, linatoa orodha ya Manjumuziki (DJ's) waliosajliwa na kuwa na vibali hai vya kufanya shughuli za sanaa hapa nchini, baraza linatoa wito kwa wadau wote wanaoendesha shughuli za sanaa na burudani nchini kuwatumia na kuwapa ushirikiano Manjumuziki (DJ's) waliopo kwenye orodha iliyotolewa.

“Ikumbukwe kwamba kufanya shughuli za sanaa bila ya kusajiliwa na kuwa na kibali ni kosa ambapo adhabu yake ni kutozwa faini isiyopungua shilingi milioni moja na isiyozidi shilingi milioni kumi. Orodha husika imeambatishwa,” imeeleza taarifa hiyo

Hatua hiyo ni sehemu ya mkakati wa BASATA wa kurasimisha sekta ya sanaa nchini na kuhakikisha wadau wote wanaofanya shughuli za ubunifu wanatambulika kisheria pamoja na kunufaika na fursa mbalimbali zinazotolewa kupitia taasisi za serikali na sekta binafsi.

Awali, Desemba 29, 2025, BASATA ilitoa taarifa ikiwataka MC na DJ wote nchini kujisajili na kuwa na vibali hai kabla ya Januari 31, 2026. Katika utaratibu huo, ada ya usajili ilipangwa kuwa Sh10,000 huku ada ya kibali ikiwa Sh40,000, hivyo mhusika alitakiwa kulipa jumla ya Sh50,000 ili kuruhusiwa kufanya shughuli zake kisheria. Katika orodha hiyo ni Ma-dj 566 tayari wamekata vibari nchi nzima.