Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Maandalizi, harusi ya Taylor Swift yapamba moto

Muktasari:

  • Swift ambaye anajiandaa kufunga ndoa na mchezaji wa Ligi ya Soka Marekani (NFL), Travis Kelce, alivutiwa na gauni hilo ambalo Elizabeth alilivaa katika harusi yake hiyo ya kwanza.

Marekani. Mwimbaji wa Marekani, Taylor Swift (36), anatarajiwa kuvaa gauni la harusi ambalo mtindo wake unafanana na lile la gwiji wa zamani wa Hollywood, Elizabeth Taylor alilovaa mwaka 1950 alipooana na Conrad Hilton.

Swift ambaye anajiandaa kufunga ndoa na mchezaji wa Ligi ya Soka Marekani (NFL), Travis Kelce, alivutiwa na gauni hilo ambalo Elizabeth alilivaa katika harusi yake hiyo ya kwanza.

Inasemekana gauni hilo la Elizabeth lilikuwa na mtindo wa kizamani uliokaa vyema kiunoni pamoja na mapambo ya lesi (lace), mambo ambayo Swift anayapenda katika uvaaji wake.

Kwa mujibu wa Daily Mail, chanzo kimoja kimenukuliwa kikisema Swift alivutiwa zaidi na mtindo huo alipokuwa akitayarisha video ya wimbo wake ‘Elizabeth Taylor’ uliopo kwenye albamu yake mpya, The Life of a Showgirl (2025).

Inaelezwa kuwa Swift alitumia muda mwingi kutazama picha za zamani za mwigizaji huyo wa filamu ya Cleopatra, jambo lililomfanya kuiga baadhi ya mitindo yake ya mavazi.

“Hivyo alipoanza kufikiria kuhusu gauni lake la harusi, alitafuta mitandaoni magauni ya zamani ya Elizabeth,” chanzo hicho kilidokeza.

Elizabeth Taylor, aliyefariki mwaka 2011 akiwa na umri wa miaka 79, alikuwa si maarufu tu kwa mafanikio yake katika filamu, bali pia kwa maisha yake ya kimapenzi yaliyovuta hisia za wengi, akiwa ameolewa mara saba katika maisha yake.

Mume wake wa kwanza alikuwa Conrad Hilton, aliyemuoa akiwa na miaka 18, lakini walitengana baada ya miezi minane tu ya ndoa. Baadaye aliolewa na mwigizaji wa Uingereza Michael Wilding (1952 - 1957) na mtayarishaji Mike Todd (1957 - 1958).

Hakuishia hapo, alikuja kuolewa na mwimbaji Eddie Fisher (1959 - 1964), mwigizaji Richard Burton (1975-1976), mwanasiasa John Warner (1976 - 1982) na fundi ujenzi Larry Fortensky (1991 - 1996).

Kwa upande wa maandalizi ya harusi, ripoti zinaeleza kuwa sherehe hiyo inatarajiwa kufanyika Julai 3 mwaka huu jijini New York, huku mialiko ya awali ikiwa tayari imetumwa kwa wageni.

Pia marafiki wa karibu wa Swift, akiwamo Selena Gomez na Gigi Hadid, wanaripotiwa kuandaa video maalum itakayochezwa siku ya harusi, ikionyesha safari ya mapenzi ya wanandoa hao tangu mwanzo.

“Sehemu kubwa ya video hiyo inaonyesha Swift akitabasamu na kucheka, kwani anafurahia sana ucheshi wa mumewe mtarajiwa Travis,” chanzo kingine kiliuambia mtandao wa The Sun.

Kwa mujibu wa Page Six, Selena atatoa burudani akiimba karaoke mbele ya wageni watakaohudhuria tukio hilo.

Swift, mshindi wa tuzo 14 za Grammy, uhusiano wake na Travis ulikuja baada ya kuachana na mchumba wake na mwigizaji kutokea Uingereza, Joe Alwyn.