Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Maarifa ajipanga kuitumia kumbukizi ya kifo cha mama yake na mashabiki

Muktasari:

  • Zawadi hiyo ambayo ni wimbo mpya atautoa siku ya kumbukizi ya kifo cha mama yake na kumbukizi ya kuzaliwa kwake Julai 22 mwaka huu

Baada ya ukimya wa takribani mwaka mmoja kwenye muziki, rapa Rashid Rais maarufu Maarifa Big Thinker amefunguka kuja na zawadi kwa mashabiki wake.

Zawadi hiyo ambayo ni wimbo mpya atautoa siku ya kumbukizi ya kifo cha mama yake na kumbukizi ya kuzaliwa kwake Julai 22 mwaka huu.

“Watu wakae mkao wa kula, Julai 22 nitatoa kibao changu cha sita siku hiyo ambayo itakuwa ni kumbukizi ya kifo cha mama yangu aliyefariki mwaka 2003 na siku yangu ya kuzaliwa,” amesema.

Hata hivyo ameeleza lengo la kutoa wimbo katika siku hiyo ni kumbukumbu katika maisha yake.

“Kwa nini nimechagua tarehe hiyo ni kwa sababu hizo ni kumbukumbu kubwa sana kwangu lakini kwa upande mwingine nimekaa mwaka mmoja na miezi sita bila kutoa wimbo wowote, nimeona niongeze kitu kingine cha tatu kwenye hiyo kumbukumbu kwa kuwapa watu kitu ambacho walikuwa wanakisubiri kwa muda mrefu,” amesema.

Pia Maarifa ameeleza sababu ya ukimya wake akidai kuna wakati maudhui peke yake hayatoshi kumburudisha shabiki.

“Kwenye muziki kunahitaji mabadiliko na utofauti kwa sababu kuna muda kutoa nyimbo nyingi kwa wakati mmoja haimaanishi watu hawatokuchoka, ifike mahali wasanii wajue kuwa maudhui peke yake hayatoshi kumburudisha shabiki hata ladha ya nyimbo pia inachangia ndiyo maana mimi tangu nimeanza muziki mpaka sasa nina nyimbo tano tu,” amesema Maarifa.

Aidha msanii huyo amefunguka mipango yake ya kutoa albamu, licha ya kuwa siku hizi wasanii wengi wanawekeza nguvu kwenye EP (Extended Playlist).

“Mipango yangu ya kutoa albamu au EP kwa sasa bado labda nikishatoa wimbo wangu mpya ndiyo nitaangalia mapokeo yakoje kama yatanifaa kutoa albamu nitatoa, kama yatanifaa kutoa EP nitatoa tu ni suala la muda,” amesema.

Utakumbuka kuwa Maarifa tangu ameingia kwenye muziki mwaka 2019 mpaka sasa ana nyimbo tano zikiwemo Karibu Kibaha, Ukiniacha, Acha Iwe aliyomshirikisha (Dogo Janja), Simshirikishi Mtu na Dhahabu.