Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Majina ya mastaa watakaohudhuria Met Gala 2026 yavuja!

Muktasari:

  • Kwa mujibu wa Page Six, Kim Kardashian, ambaye ni mgeni wa kudumu wa hafla hiyo, anatarajiwa kurejea tena mwaka huu. 

Marekani. Orodha ya wageni mashuhuri wanaotarajiwa kuhudhuria Met Gala 2026 itakayofanyika Jumatatu ya kwanza ya Mei imeanza kuvuja, huku majina makubwa yakitajwa kuwa yataonekana kwenye zulia jekundu la tukio hilo kubwa la mitindo.

Kwa mujibu wa Page Six, Kim Kardashian, ambaye ni mgeni wa kudumu wa hafla hiyo, anatarajiwa kurejea tena mwaka huu. 

Hata hivyo, bado haijajulikana kama Kendall Jenner pamoja na dada zake wengine na mama yao, Kris Jenner watahudhuria kama ilivyokuwa miaka iliyopita.

Met Gala ni hafla kubwa ya kimataifa ya mitindo inayofanyika kila mwaka jijini New York, Marekani, hasa katika makumbusho ya sanaa ya Metropolitan.

Inajulikana kama tukio la kifahari na la kuvutia zaidi duniani na lenye mkusanyiko mkubwa zaidi wa mitindo.

Lilianzishwa mwaka 1948 na Eleanor Iambert, huandaliwa na Jarida la vogue likihusisha watu maarufu au watu wenye umuhimu kitamaduni kutoka nyanja mbalimbali kama siasa, filamu michezo, mitandao ya kijamii n.k.

Hufanyika kila Jumatatu ya kwanza ya mwezi Mei (kasoro mwaka 2021 ilifanyika Septemba baada ya kusimamishwa kutokana na janga la Covid 19) na huwa kuna kiingilio ambacho kufikia hadi Dola75,000, wastani wa Sh187 milioni. 

Hata hivyo, hii si hafla ya yeyote kwenda na kuibukia tu katika zulia jekundu, wageni huchaguliwa na Anna Wintour ambaye ni Boss wa Vogue, na tiketi zake ni ghali sana na mara nyingi hugharamiwa na chapa za mitindo.

Tukio hili hulenga kuchangisha fedha kwa ajili ya taasisi ya Costume Institute ambayo ni kitengo maalum cha makumbusho ya Metropolitan kinachohusika na mitindo ya mavazi kama sanaa, na wao ndio huamua Met Gala iweje katika mwaka husika.

Kazi ya taasisi hiyo ni kukusanya na kuhifadhi mavazi ya kihistoria na ya kisasa, na kubwa zaidi wao ndio wanapanga maonyesho ya mitindo kila mwaka yafananaje (theme) kwa waalikwa wote.

Taarifa zinaeleza kuwa mwigizaji Julia Garner pia atakuwapo mwaka huu, sambamba na mbunifu na mwanamitindo Alexa Chung, Gabrielle Union, Rebecca Hall, pamoja na mchezaji wa Golden State, Warriors Jimmy Butler.

Aidha, mwanamitindo na mfanyabiashara wa bidhaa za urembo, Hailey Bieber anatarajiwa kuhudhuria, ingawa bado haijathibitishwa kama mumewe Justin Bieber atakuwapo katika hafla hiyo.

Hata hivyo, waandaaji bado hawajatoa orodha rasmi ya mwisho ya wageni watakaohudhuria tukio hilo kubwa la kimtindo duniani.
Akizungumza na Vogue, msimamizi wa Costume Institute, Andrew Bolton alisema, “Kinachounganisha kila idara ya uandaaji na kila ukumbi wa maonyesho ndani ya makumbusho ni mitindo.

Hilo ndilo linaunganisha kila kitu ndani ya makumbusho, na ndilo lilikuwa wazo la awali la maonyesho haya.”

Maonyesho hayo yanatarajiwa kuhusisha takribani mavazi na vifaa 200 yakioanishwa na kazi za sanaa 200, hatua inayolenga kuonyesha uhusiano wa moja kwa moja kati ya ubunifu wa mavazi na sanaa. 

Kamati ya waandaji wa hafla hiyo inajumuisha majina makubwa kama Beyonce, Nicole Kidman, Venus Williams, na Anna Wintour.

Mbunifu wa YSL, Anthony Vaccarello pamoja na mwigizaji Zoe Kravitz wanaongoza kamati ya wenyeviti, huku ikijumuisha pia wasanii na watu mashuhuri kama Sabrina Carpenter, Doja Cat, Gwendoline Christie, Alex Consani, Misty Copeland, Elizabeth Debicki, Lena Dunham, Paloma Elsesser, LISA, mhariri mpya wa Vogue Chloe Malle, Sam Smith, Teyana Taylor, Lauren Wasser, Anna Weyant, A’ja Wilson, na Yseult.