Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mama Hamisa kutoka kilo 165 hadi 85

MOBETTO Pict

Muktasari:

  • Mama Hamisa amesema amepunguza kilo kutoka 165 na sasa ana 85 katika miezi 10 tangu afanyiwe upasuaji Dubai na sasa anadunda kama kawa.

Dar es Salaam. Baada  ya hekaheka za harusi ya mwanaye Hamisa Mobetto na mumewe Stephane Aziz Ki, mama wa mrembo huyo ameamua kufunguka kupungua kwake mwili baada ya watu wengi kumshangaa wakati wa sherehe hiyo, wakidhani ni tatizo kiafya.

Mama Hamisa amesema amepunguza kilo kutoka 165 na sasa ana 85 katika miezi 10 tangu afanyiwe upasuaji Dubai na sasa anadunda kama kawa.

Amesema ameamua kuyasema hayo kutokana na wengi kutaka kufahamu kabla ya upasuaji alikuwa na kilo ngapi, aina ya upasuaji aliofanya na anajisikiaje kwa sasa baada ya mabadiliko hayo.

"Kwanza kabisa nilipoanza kuonekana mwili wangu umepungua katika kwenye harusi ya mwanangu Hamisa, watu wengi walishtuka na kuniuliza nini kimenitokea, sikutaka kuzungumzia hili kwa urefu, nilisubiri hekaheka ziishe halafu ndiyo nije kuwaelezea watu juu ya mwili wangu na ndiyo maana hata ulivyoniuliza sikufunguka sana.

"Hapa unaponiona zimepungua kilo 80 ndani ya miezi 10 tangu nilipofanyiwa upasuaji, yaani mwanzo nilikuwa na kilo 165 sasa hivi nina kilo 85.

"Mimi bwana nimefanya upasuaji aina ya Gastric Bypass kwa kiswahili ni upasuaji wa kupunguza uzito unaofanywa kwenye tumbo na mfumo wa chakula, yaani tumbo linapunguzwa na sehemu ya utumbo mdogo inapitiwa ili kupunguza ufyonzaji wa chakula na hii husababisha mtu kushiba haraka na kula kidogo," amesema Mama Hamisa.

Amesema aliamua kufanya upasuaji huo baada ya kujaribu njia nyingi kama mazoezi, kupunguza kula na kumeza dawa bila mafanikio ya kudumu.

"Yaani upasuaji ulichukua muda mfupi na hospitali nilikaa siku chache tu, hadi kupona kabisa nilitumia wiki kadhaa. Kuna maumivu kidogo mwanzoni nilikuwa nayasikia, lakini kwa msaada wa madaktari na kufuata ushauri, kila kitu kilikwenda salama na sasa nadunda, kazi ipo kwenye kufanya nidhamu, mpangilio wa chakula na mazoezi mepesi," alisema.

Amesema kwa sasa anasikia furaha kwani akiwa na mwili mnene ilifikia hatua mbaya kutokana na kujiachia kwa kula kila kitu vikiwamo vyakula vya kuongeza uzito.

"Huu mwili ndiyo niliokuwa nauhitaji, ule unene na uzito kwa kweli nilikuwa naelekea kubaya, nashukuru Mungu kufika hapa na kuhusu watu wanavyonizungumzia ikiwemo kusema naumwa, mara nina 'stress' sijali kwani hata nilivyokuwa mnene hao hao walikuwa wananisema na kunipa maneno mengi tu," amesema.