Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mawakili washtukia njama za kumuua R Kelly gerezani

Muktasari:

  • Mawakili R Kelly wanadai kuwa kuna ushahidi wa wazi unaowalenga maofisa wa polisi kupanga njama ya kumuua mteja wao ambaye anatumikia kifungo cha miaka 30.

Timu ya wanasheria wa msanii wa R&B, Robert Sylvester  maarufu R. Kelly, imewasilisha ombi la dharura kutaka msanii huyo aachiwe mara moja kutoka gerezani na apewe kifungo cha nyumbani, hii ni baada ya kudai maisha yake kuwa hatarini katika gereza hilo.

Mawakili hao wanadai kuwa kuna ushahidi wa wazi unaowalenga maofisa wa polisi kupanga njama ya kumuua R. Kelly katika gereza la Serikali huko North Carolina, ambapo anatumikia kifungo cha miaka 30.

Katika ushahidi wao, waliwasilisha tamko la kiapo kutoka kwa Mikeal Glenn Stine, mfungwa anayetumikia kifungo cha maisha (terminally ill), ambaye alidai kuwa maofisa wa gereza walimshawishi amuue R. Kelly kwa ahadi ya kuachiwa huru.

Stine aliambiwa kuwa R. Kelly na mawakili wake walikuwa karibu kufichua taarifa za kuumiza kuhusu ukiukwaji wa haki, zikiwemo madai ya maofisa kuingilia mawasiliano binafsi kati ya mteja na wakili wake.

Aidha aliweka wazi kuwa maofisa walimwambia akikamilisha agizo hilo atashtakiwa kwa mauaji ya R. Kelly, lakini ushahidi utakaotolewa hautashughulikiwa na hakutakuwa na hatia.

Inaelezwa kuwa, Stine alianza ukaribu na R. Kelly Machi 2025 na alikuwa tayari kumuua lakini alibadili uamuzi wake na kumfungukia R. Kelly kwamba maofisa wa Ofisi ya Magereza walimuagiza kutekeleza mauaji yake.

Wakili wa R. Kelly anadai kwamba Juni mwaka huu, walishtuka kuhusu mfungwa mwingine aliyetumwa na maofisa kuwaua R. Kelly na Stine ambapo wanadai kuwa R. Kelly yuko hatarini kwa kuwa bado yuko kifungoni gerezani hapo na wafungwa wengine ambao wanaweza kutumika kutekeleza mauaji yake.

“Tishio kwa maisha ya Kelly linaendelea kila siku kwamba hakuna hatua zinazochukuliwa, wafungwa zaidi ya wawili waliagizwa kumuua. Zaidi ya mmoja tayari amefikishwa kuhusu kutekeleza mauaji yake. Mmoja wao atafanya kile ambacho Stine ameshindwa, hivyo kuzika ukweli kuhusu kile kilichotokea katika kesi hii pamoja na Robert Kelly,” mawakili waliandika kwenye jalada hilo.

Wakili wa R. Kelly, Beau B. Brindley, anamuomba hakimu wa mahakama amuachilie msanii huyo atumikie kifungo cha nyumbani angalau kwa muda mfupi.

Mwimbaji huyo alitiwa hatiani kwa makosa tisa ambapo Septemba 2021 alishtakiwa kwa kukiuka sheria na ulaghai uliohusisha unyanyasaji wa kingono kwa watoto.

Juni 2022, alihukumiwa kifungo cha miaka 30 gerezani. Pia, Februari 2023, R. Kelly alihukumiwa kifungo cha miaka 20 jela kwa makosa ya uhalifu wa kingono kwa watoto, huku hakimu akiamua kwamba muda wote isipokuwa mwaka mmoja atatumikia kwa wakati mmoja na kile kifungo chake cha awali cha miaka 30.

Hata hivyo, Februari 2025, mahakama ya rufaa iliidhinisha hukumu ya R. Kelly ya ulaghai na ulanguzi wa ngono pamoja na kifungo chake cha miaka 30 jela. Pia, mahakama hiyo ilikataa madai yake kwamba ushahidi wa kesi haukutosha na kwamba hakimu wa kesi hiyo alitoa uamuzi usiofaa.