Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mdomo wa Kanye West wageuka gumzo

Muktasari:

  • Utofauti huo umegundulika siku ya jana baada ya kusambaa video katika mitandao ya kijamii zikimuonesha Kanye akieleza kuhusiana na haki aliyonayo juu ya kuposti picha za mkewe Bianca Censori.

Marekani. Ikiwa umepita mwezi mmoja tangu mwanamuziki Kanye West kuweka meno ya 'grili' yaliyotengenezwa kwa madini ya Titanium kwenye kinywa chake, mashabiki wamegundua utofauti kwenye mgomo wa juu wa rapa huyo.

Utofauti huo umegundulika siku ya jana baada ya kusambaa video katika mitandao ya kijamii zikimuonesha Kanye akieleza kuhusiana na haki aliyonayo juu ya kuposti picha za mkewe Bianca Censori.

Katika video hiyo inaonesha sehemu ya juu ya mdomo wa Kanye ukiwa umevimba, jambo lililopelekea  mashabiki kuhoji kilichosababisha utofauti kwenye mdomo wa mwanamuziki huyo.

Aidha kwa mujibu wa Website ya Page Six, imefanya mahojiano na daktari kutoka New York, Clement Kairouz ameeleza kuwa uvimbaji kwenye sehemu hiyo ya mdomo unatokana na 'grili' alizoziweka kusukuma mdomo wa juu wakati Kanye akiongea.

Ikumbukwe kuwa Januari , 2024 Kanye West aliweka grili za madini ya Titanium, zenye thamani ya dola za Marekani 850000 zaidi ya Sh2.1 bilioni kwenye meno yake.