Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Ndani ya boksi: 'Fleva’ ya Sinza haipo tena

Muktasari:

  • Hii ndo ilimfanya Gwiji la Bongo Fleva Profesa Jay. Aseme “Sinza ya leo kila banda ya nyumba bar”. Yes! Bar zilikuwa nyingi kuliko ‘famasi’, ‘steshonarizi’, vituo vya mafuta na maduka ya nguo. Kwa kifupi upimbi huu haukuwapo.

Dar es Salaam. Siku ya Ijumaa kutoka Shekilango hadi Bamaga. Kulia na kushoto ungeona ndinga zimepaki kando ya barabara. Bar, Pub, Grosare, Salon, taksi na pisi zikipitapita. Hii ndo Sinza niijuayo tangu na tangu.


Hii ndo ilimfanya Gwiji la Bongo Fleva Profesa Jay. Aseme “Sinza ya leo kila banda ya nyumba bar”. Yes! Bar zilikuwa nyingi kuliko ‘famasi’, ‘steshonarizi’, vituo vya mafuta na maduka ya nguo. Kwa kifupi upimbi huu haukuwapo.


Kutoka Rombo Green View, Kili Time, Legho, Kamanyora, Miti Mitatu zote hizo bar. Unaibukia Mugabe kulia bar na kushoto bar, kisha ungeingia Sinza Madukani. Hapo kulikuwa na pub, ‘grosare’ na maduka, bar hadi uingie ndani zaidi.


Kwa sasa Madukani hapana tofauti na mitaa ya Tandamti na Narung’ombe. Mazingira ya eneo hili hayana tofauti na Kariakoo. Kimsingi ni ‘kopi na kupesti’ ya kile kilichopo Kariakoo. Hakuna mwenyeji wote waja asubuhi na kusepa usiku.


Na kuanzia maeneo haya ndipo ungeanza kuiona ‘testi’ ya Sinza. Sinza ilikuwa tofauti na maeneo mengine kwa viti vingi. Watoto wa kiume na wa kike walikuwa wajanja. Banza Stone akaibatiza kama Sinza kwa Wajanja.


Baada ya madukani ungekutana na salon za kike kibao, kabla ya kuingia Sinza Kijiweni. Hapo kati ungekutana na pisi zenye ‘fremu’ za huduma ya ‘intaneti’, urembo na ‘photokopi’. Wazuri, wabichi, laini na wadogo wadogo.


Kwa sababu wengi wao waliishi na wazazi wao. Walikaa kwenye nyumba za familia. Kutoka kwa kina Diana wa Sinza Vatcan hadi kwa Cecilia wa Sinza Lion. Hapo kati ungekutana na pisi zilizojaa sifa za kimalaika tupu.


Baada ya Sinza Kijiweni inafuata Sinza Kumekucha. Kuna tofauti ya Kijiweni na Kumekucha. Hapa Kumekucha barabarani kulikuwa na maduka zaidi. Lakini ukiingia kushoto kulikuwa na bar zimejaa hadi Travertine Hotel. Achana na shule na kanisa.


Ukiingia kulia unaenda kutokea Lion Hotel. Kabla ya kuifikia hiyo Lion, lazima ukutane na watoto wa kike wazuri wenye malezi na makuzi ya kifamilia. Wanatokea majumbani kwao, hawakutokea ‘gesti’ kama wasichana wa Sinza ya leo. Uliza uambiwe.


Sinza hii asilimia 100 wapangaji. Wa vyumba, frem ama ‘gesti’, ni ngumu kukutana na msichana akiishi Sinza kwa wazazi. Katika 100 utapata mmoja, wengi wao hutokea geto kwake, kwa masela wake. Kimsingi Sinza imepoteza ile ladda ya Sinzani.


Pisi nyingi ukiziona mchana ujue muuzaji au mteja duka la nguo. Mhudumu vibanda vya miamala au kafuata msosi wa visinia sijui au anadanga. Wenyeji wamebaki wachache sana wengi wageni na wapo kibiashara au kihasara tu.


Kibiashara ni kumiliki ‘frem’ ya duka, bar, pub, ‘grosare’ kama sio salon. Waliopo kihasara ndo wale mchana kutwa amejilaza ‘loji’ au ‘gesti’. Usiku anachomoka na kwenda kutafuta hela ya kula na kulipa pale ‘loji’. ‘Naiti shifti’.


Ukitoka Kumekucha unazamia Sinza Palestina. Kwa asili yake hapa kulikuwa na ‘Famasi’ flan hivi, kwa sababu kando yake ipo hospitali. Lakini sasa hivi kuna maduka mengi kuliko pale Sinza Madukani au Mwanjelwa. Noma sana.


Sehemu pekee ambayo imetunza asili yake ni Sinza Makaburini. Na ukifika bila kuangalia upande wa makaburi huwezi kujua kama ni Sinza Makaburini. Maana frem kama zile za mitaa ya Samora Posta. Hakuna Gaza Bar wala Tel Aviv Bar imebaki Mwika tu.


Banda ya Makuburini utaingia kwa Remmy. Sinza kwa Remmy hadi Mori, kuna madude flan yameenda hewani. Hakuna cha B Bar wala Miller Bar. Hakuna cha Texas Salon wala Azania ‘Gesti’. Kwanza hata kujua ilipo nyumba ya Dr Remmy ngumu sana.


Hapo Mori ukizama mida ya ‘naiti naiti’, utadhani upo Tokyo. Zama zile kulikuwa na mbuga flan ya wadudu wa kupiga mikasi. Sasa ni mwendo wa maduka matupu kama Times Square New York. Ni wazi ‘testi’ ya Sinza imetoweka kabisa.


Kuna mwingiliano hatari. Kuanzia Mori hadi Africa Sana. Kitambo kile ulikuwa ukanda wa wadudu wa mikasi. Leo hii wamefunikwa na River Side, ile michongo Sinza imehamia kwenye mabar mabar makubwa tu. Ambako gharama ya totozi ni kubwa.


Bar maarufu Sinza ilikuwa Delux, Mawela, Vatcan, T Garden, Lion, Mseri Bar, Gaza Bar, Miller Bar, B One, Mori Bar, Meeda Bar, Soccer City Bar, Lillys Bar na Corner Bar. Zipo pub na grosare nyingi sana na idadi yake ngumu kukumbuka zote. Leo Bar kubwa kubwa ni nyingi kuliko daladala.


Barabara za mitaa zimejengwa kuliko zamani. Lakini ‘testi’ ile ya Sinza Sinzani haipo yena. Yaani imekuwa kama chupa ya zamani isiyo na mvinyo. Mitaani hakuna pisi za kishua zimejaa zile pisi za kujichubua. Zilizokosa mlo sahihi kama binadamu.


Zamani hata kiswahili cha Sinza kilikuwa daraja tofauti na eneo lingine. Sinza ilikuwa uswanglish mwingi yaani mabloo wa Sinza walijikuta kina Nas, Snoop, Jay Z na Bin Pun. Lakini hivi sasa kwa matamshi tu, ni ngumu kujua upo Sinza ama Manyoni.