Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Ndani ya Boksi: Nora, Sinta, Nina na Kissa!

Muktasari:

  • Wakiwa kwenye kilele cha juu cha mafanikio yao. Vikaibuka vikundi vingine kadhaa vikiwa na wasanii vichwa pia. Lakini leo nitatambaa na Kundi la Kaole tu. Hapo kuna Kissa, Nora, Sinta na Nina. Kiumeni akiwepo Dk Cheni, Mashaka, Muhogo Mchungu na wengineo.

Dar es Salaam. Achana na Waridi. Kuna Aisha na Natasha. Achana na Monalisa. Ni kwamba hawa walikuwa alama sahihi ya sanaa ya uigizaji nchini. Kiumeni wakiwepo kina Sumbi na Bocha, Bishanga, Rich Richie na wengineo. Dar es Salaam ilikaa kimya Mambo Hayo ikiruka kwa hewa. 

Wakiwa kwenye kilele cha juu cha mafanikio yao. Vikaibuka vikundi vingine kadhaa vikiwa na wasanii vichwa pia. Lakini leo nitatambaa na Kundi la Kaole tu. Hapo kuna Kissa, Nora, Sinta na Nina. Kiumeni akiwepo Dk Cheni, Mashaka, Muhogo Mchungu na wengineo.

Leo sitaki kugusa masela nataka ‘kudili’ na pisi za kitambo. Majina kama Nora, Nina, Sinta, Kissa na baadaye zikaibuka sura kibao za wasanii wapya. Waliokuja baada yao wameendelea kukomaa na gemu. Lakini hao vichwa wa kale ni kama waliamua kulikataa na gemu lenyewe.

Kwanini? Walishindwa kuvumilia ili waje kula mbivu. Ama mbivu za nje ya sanaa zimewashibisha sana? Nora kwanini alilipa kisogo ‘gemu’? Nina je? Sawa, Sinta je? Kissa alikosewa nini na sanaa hii iliyobadilisha maisha ya madem wengine wengi nchini? Akasusa.

Kama ulikuwepo Nina akiwa pale juu. Kama ulishuhudia ustaa wa Nora yulee? Kama ulikuwa mdau wa sanaa nyakati za Sinta kweli. Bila shaka utakubaliana na mimi kwamba kati ya sanaa na hawa wasanii, kuna mmoja anadaiwa na mwenzake. Wasanii wanadai au sanaa inawadai?

Aisha alimfanya Nora atamani kazi ya uigizaji. Waridi alimfanya Kissa atamani kazi ya kuigiza. Na hawa kina Nora wakamfanya Johari atoke Shinyanga kuja Dar kwa kazi ya uigizaji. Kinachotupa shaka ni kwanini waliowapa ari  ya kufanya sanaa, wao wako nje ya sanaa? Kwanini? 

Sinta aliyemfanya Wolper awe muigizaji, yeye kalikimbia gemu? Je, sanaa haikuletei uhakika wa maisha au maisha ndo hayakupi uhakika wa sanaa? Wanaojisifu kufanikiwa kwa sanaa hivi sasa, tuendelee kuwaamini maneno yao? Kama inalipa kwanini wao wameikwepa? Ama uzee?

Morgan Freeman, Robert De Nero, Danzel Washington, Will Smith, Angeline Jolie, Vivica Fox na hata Stallone ‘Rambo’. Uzee wao umewakuta wakiwa mzigoni ‘lokesheni’. Kuna vibabu na vibibi vingi kule Hollywood, vimezaliwa na kuzeekea kwenye sanaa. Vipo mpaka leo vikicheza ‘sini’ zenye umri wao.

Kwa sababu uigizaji ni kazi ya utotoni hadi uzeeni. Utaigiza kama mtoto, kama kijana, kama mzee na ‘samtaim’ kama mzuka ukitangulia mbele ya haki. Hawa kina Nora wakati wanatemana na sanaa walikuwa masista duu tu . Waliacha ghafla kama chafya za kiangazi. Kwanini?

Sanaa iliwaondoa mstarini ama wao waliiondoa moyoni mwao? Kuna kundi la wasanii walio nje ya ulingo, wenye ubora kuliko walio ndani ya ulingo hivi sasa. Mtazame Aisha, Waridi, Kemmy au Sauda Kilumanga. Ni kwanini wamejitenga? Hawataki kuigiza na makunyanzi ya uzee usoni?

Bongo tu au Afrika nzima? Kuna ‘sini’ ngapi zinataka mwanamke umri wa Aisha? Umri wa Sinta au Nora? Inawezekana Nina yeye alitemana na sanaa kwa sababu ya matakwa ya mume. Vipi hawa kina Mainda na Johari? Ni kweli wanatakiwa kukaa nje ya sanaa? Ama sanaa ya Bongo haina urafiki na uzee?

Bongo Fleva wamekuwa na kitu flan cha kuwakumbuka wasanii wakongwe. Kuna juhudi kubwa inafanywa na wadau kuwafanya wanamuziki wa kitambo wawe katika ramani. Wasomeke kama siyo kujipatia riziki hata uzeeni kwao. Lakini sanaa ya uigizaji ni kama inatengana na wakongwe. Haiwataki au hawaitaki.

Taratibu ni kama wanatemana na kina Kajala. Maana wanakimbiza zaidi kwenye uhusiano kimapenzi kuliko kisanaa. Kajala wa Konde zaidi kuliko Kajala wa filamu na tamthiliya. Shida ni nini? Anti wa sasa anasifika kwa mengineyo na siyo sanaa yake. Ndivyo ilivyo hata kwa Wema, Wolper, Uwoya na kina Lissa.

Tunalazimisha wazeeke au wao ndo wanajizeesha? Sanaa gani ina wastaafu? Sanaa ni kama vile mvinyo, unavyoishi muda mrefu ndivyo unazidi kuwa mtamu na imara. Sanaa au wasanii husika kuna kimoja ‘kinakimisi’ kingine. Hatuwezi kustaafisha wasanii kila siku, wakati sanaa inahitaji watoto hadi vikongwe.

Michezo ya kususia sanaa ilianza kitambo. Bishanga ni mmoja wa wasanii wa mwanzo waliosusa kufanya mchongo huu. Mjomba Fujo na wengineo walitemana na sanaa mapema sana. Nani kati ya sanaa na wasanii anayekerwa na mnzake? Ama mpaka uwe msanii ili ujue kero ya sanaa pindi ukii hia uzeeni?

Leyla Visram alihitaji kuigiza na Waridi ili awe bora zaidi. Kama Lulu alivyoigiza na Dk Cheni au Kanumba na JB. Leo hii msanii mpya anafanya kazi na msanii mpya. Yaani Leyla anategemea kujifunza kwa Nana Dollz? Nana anayepaswa kuusoma mchezo kupitia kwa Kemmy. Ni kama mtoto kulea mtoto.

Balaa la Monalisa halikutokea kwa bahati mbaya. Aliingia katika sanaa katikati ya mafundi kweli. Alishikwa na mamake Natasha, kando yake kuna Waridi, Aisha, Bishanga, Rich Richie na kubwa kuliko akiongozwa wa mumewe Tyson. Ndicho kilichomtokea na Rose Ndauka.

Rose Ndauka naye ni kama vile sanaa kaikataa jumla. Naye ni mmoja wa wasanii waliopitia katika mikono sahihi. Filamu ya Swahiba ndiyo iliyomtoa kisanii. Ikimilikiwa na wakongwe wawili JB na Rich. Hawa walimjenga Rose huyu tunayemjua sasa. Hiki kitu hakipo kwa Leyla Visram na wenzake. Ni yatima.

Inawezekana ama ndo ukweli. Sanaa ni daraja la kukutafutia njia ya kwenda sehemu sahihi. Lakini siyo kazi ya kukutafutia kipato kikubwa. Ndo maana waliojipata wanaikataa. Sinta, Nora, Nina, Kissa, Bishanga, Waridi, Aisha na kina Kemmy. Walitumia sanaa kupata kazi sahihi ya kuwapa maisha sahihi?
Nakataa.