Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Nedy Music: Kuingia kwenye fashion hakunizii kufanya muziki

Muktasari:

  • Kama ambavyo wamefanya wasanii wengine ndivyo pia mwanamuziki Bongo Fleva Said Seif Ally ‘Nedy Music’ siku za hivi karibuni licha ya kuwa anaendelea na muziki lakini ameonekana kwenye upande wa fashion jambo lililosababisha maswali kwa baadhi ya mashabiki wake.

Dar es Salaam, Kwenye kiwanda cha burudani Bongo imekuwa kawaida wasanii kufanya kazi ya sanaa zaidi ya moja yaani mwigizaji anaweza kuwa mwimbaji pia kama ilivyo kwa baadhi ya wasanii akiwemo Lulu Diva, Quick Racka, Romy Jons na wengineo

Kama ambavyo wamefanya wasanii wengine ndivyo pia mwanamuziki Bongo Fleva Said Seif Ally ‘Nedy Music’ siku za hivi karibuni licha ya kuwa anaendelea na muziki lakini ameonekana kwenye upande wa fashion jambo lililosababisha maswali kwa baadhi ya mashabiki wake.

Akizungumza na Mwananchi mwanamuziki huyo ameeleza maisha yake kwenye upande wa fashion.

“ Nadhani hakuna sababu rasmi ya mimi kujikita katika fashioni kwa sababu ukinizungumzia mimi upande wa sanaa tu kwa maana ya music tayari unazungumzia fashion kwa sababu ipo ndani yake, kila siku tuna-shoot video na kufanya show ambazo zinahitaji uvae nguo kuendana na fashion,” amesema

Hata hivyo ameeleza kuwa fashioni ipo ndani yake na haimzuii yeye kufanya muziki kwa sababu muziki pia unaitaji fashion.

“Haimaanishi mimi kwenda na fashion au kuwepo kwenye fashion kunizuie kufanya muziki wangu kwani mavazi yanabeba muonekano wa msanii kwa hiyo fashion iko ndani yangu na ina kuwepo katika mzunguko wa kila siku” amesema Nedy.

Aidha amezungumzia kilichofanya aonekane kwenye baadhi ya matukio ya fashion ikiwemo Miss Kinondoni , 

“Wakati mwingine naenda kwenye event kubwa za fashion kwa sababu mimi tayari ni mtu maarufu ambaye naweza kutumika kwa namna moja ama nyingine kwenye kuhamasisha masuala ya fashion au kuitangaza kwa hiyo kuniona pale kuna kuwa kuna vitu vingi zaidi” amesema.

Kwa nini sasa hivi hatoi ngoma back to back ?

“Back to back ziliweza kutoka na ulikuwa wakati mzuri ni mipango tu ya namna ambavyo naweza kwenda na mashabiki kwa sababu uzuri wana-support kila leo na bado naendelea kutoa project hata kama zinapishana,” amesema.

Aidha ameeleza namna ambavyo tasnia ya muziki inavyokuwa kwa kasi ikilinganishwa na wakati alioanza muziki.

“ Tasnia ya muziki inakuwa siku hadi siku kulingana na miaka ambayo mimi niliingia ambapo ukuaji huo mpaka sasa unatokana na vizazi vimekuwa tofauti tofauti,” amesema.

Afunguka changamoto za sasa katika muziki

Hata hivyo Nedy ameweza kufunguka changamoto wanazokumbana nazo wasanii kwa sasa katika muziki kwa kudai hivi sasa kila mtu ana ujuzi wa kutengeneza muziki mzuri.

“Changamoto zipo ila siyo kubwa kwa sababu siku hizi kila mtu yupo na ujuzi ila kitu ambacho nafurahia kuona hata wanamuziki wachanga wamekuwa watu ambao wanafanya vitu vizuri na vikubwa vinavyoleta ushindani japo kuna changamoto nyingine kubwa na haziwezi kuzuilika” amesema.

Kipaumbele chake kati ya muziki na fashion?

Nedy ameeleza kuwa fashion na muziki vyote anavifanya kwa pamoja kwa sababu ni vitu ambavyo vinatemeana.
“Vyote navipa kipaumbele ni vitu ambavyo vina tegemeana na watu watarajie mazuri kupitia hivyo”

Mwanamuziki huyo amewahi kufanya nyimbo kama Rudi, Pinda, Nishalewa, Tiamo, Carino, Amesahau, Kinoma noma na nyingine nyingi.