Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Rayvanny afunguka baada ya kutoka Canada, Kombe la Dunia 2026 

Muktasari:

  • Akizungumza baada ya kuwasili nchini Rayvanny amesema baadhi ya watu walibeza na kutilia shaka uwezo wake baada ya kutangazwa kuwa miongoni mwa wasanii watakaotumbuiza kwenye tamasha hilo. Amesema aliamua kukaa kimya na kuacha matendo yaongee

Dar es Salaam. Msanii wa Bongo Fleva, Raymond Mwakyusa 'Rayvanny', usiku wa kuamkia leo amewasili nchini akitokea Toronto, Canada, alipokwenda kushiriki tamasha la Countdown kuelekea ufunguzi wa Kombe la Dunia 2026. 

Akizungumza baada ya kuwasili nchini Rayvanny amesema baadhi ya watu walibeza na kutilia shaka uwezo wake baada ya kutangazwa kuwa miongoni mwa wasanii watakaotumbuiza kwenye tamasha hilo. Amesema aliamua kukaa kimya na kuacha matendo yaongee.

"Endeleeni kunichukulia poa tu, mimi nafanya matendo tu," amesema Rayvanny

Msanii huyo amesema amejivunia kuiwakilisha Tanzania katika moja ya majukwaa makubwa zaidi duniani. Akieleza kuwa mafanikio hayo si yake binafsi bali ni ushindi kwa muziki wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla.

Amesema alijisikia fahari kuona bendera ya Tanzania ikipepea mbele ya maelfu ya mashabiki kutoka mataifa mbalimbali, waliokusanyika kushuhudia shamrashamra za kuelekea Kombe la Dunia.

Katika tamasha hilo, Rayvanny aliandika historia kuwa miongoni mwa Watanzania wachache kupata nafasi ya kutumbuiza kwenye matukio yanayohusishwa na Kombe la Dunia. Alipanda jukwaani pamoja na mastaa mbalimbali akiwemo Nora Fatehi. Huku burudani yao ikipokelewa kwa shangwe kutoka kwa mashabiki.

Akizungumzia uzoefu alioupata, Rayvanny amsema hatua hiyo inaonyesha kuwa muziki wa Tanzania una uwezo mkubwa wa kufika mbali zaidi, endapo wasanii wataendelea kufanya kazi kwa bidii na kutumia vizuri fursa za kimataifa.

Kwa mujibu wa msanii huyo, kupanda jukwaa hilo ni ishara kwamba Bongo Fleva imeendelea kupata heshima na kutambuliwa katika majukwaa makubwa duniani.

Mbali na safari yake, Rayvanny pia aligusia mijadala mbalimbali inayoendelea kwenye tasnia ya muziki nchini kama mahusiano ya Diamond na Harmonize

"Diamond na Harmonize wanapendana sana. Walipishana njia, lakini bado ni jambo ambalo linawatesa ndani kwa ndani mpaka leo," amesema.

Kuhusu msanii Macvoice, Rayvanny amesema ameamua kubeba lawama na kuonekana mbaya mbele ya watu ili kuhakikisha kijana huyo anakuwa salama na anaendelea vizuri na maisha yake ya muziki.

Amesema upendo alionao kwa Macvoice ni mkubwa kiasi kwamba yuko tayari kukosolewa na baadhi ya watu, ikiwa hilo litamsaidia msanii huyo kupata utulivu na kuendelea kujijenga kisanii.

Ushiriki wa Rayvanny kwenye tamasha la Countdown to World Cup 2026 umeongeza rekodi ya mafanikio ya msanii huyo ambaye katika miaka ya karibuni, amekuwa akifanya maonesho katika mataifa mbalimbali na kushirikiana na wasanii wa kimataifa. Hatua iliyosaidia kuutangaza zaidi muziki wa Tanzania nje ya mipaka yake.